Kenya yanakili ongezeko la asilimia 73 la mauzo ya parachichi

Kenya iliuza ng’ambo tani elfu 26 za zao la parachichi kati ya mwezi Januari na Machi mwaka huu, kiwango ambacho ni ongezeko la asilimia 73 la mwaka.

Takwimu za hivi punde kutoka Idara ya Kilimo cha bustani zinafichua kwamba mauzo ya parachichi wakati wa miezi ya Januari hadi Machi yaliwapa wakulima mapato ya shilingi bilioni 4.2.

Also Read
WHO yahimiza raia kuvaa barakoa wakati wa sherehe za Krismasi

Kulingana na idara hiyo, kiwango cha uzalishaji zao hilo kimeongezeka kutokana na ukuzaji wa parachichi katika maeneo ambayo awali hayakukuza zao hilo kama vile Bonde la Ufa na maeneo mengine ya Magharibi mwa Kenya.

Also Read
Marufuku ya Kenya ya kuuza maembe Ulaya kuondolewa Septemba

Aidha mauzo ya parachichi yameongezeka kutokana na ongezeko la mahitaji yake katika mataifa ya Mashariki ya Kati na Ulaya.

Hata hivyo idara hiyo imesema maua ndiyo yanailetea sekta hiyo pato kubwa.

Also Read
Bara la Ulaya laongeza juhudi za kukabiliana na maambukizi ya COVID-19

Kenya iliuza ng’ambo tani 50 za aina kadhaa za maua na kupata mapato ya zaidi ya shilingi bilioni 32 katika kipindi hicho.

Wakati wa kipindi hicho, nchi hii iliuza mboga za thamani ya shilingi bilioni 8.2.

  

Latest posts

Mauaji ya mwanaume mmoja yazidisha taharuki Ol Moran

Tom Mathinji

IEBC kuongeza Idadi ya nchi za ugenini ambako wakenya watashiriki kwa upigaji kura

Tom Mathinji

COVID-19 yavuruga mbinu za upangaji uzazi hapa nchini

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi