Kenya yanakili visa 12 zaidi vya Covid-19

Kenya imenakili visa vingine 12 vya maambukizi ya ugonjwa wa Covid-19 katika muda wa saa 24 zilizopita, baada ya kupimwa kwa sampuli 763, huku kiwango cha maambukizi ya virusi hivyo kikitimia asili mia 1.6.

Idadi jumla ya waliothibitishwa kuambukizwa ugonjwa huo hapa nchini sasa ni  watu 337,950, kutoka kwa idadi jumla ya sampuli   3,838,211 zilizochunguzwa tangu mwezi Machi mwaka 2020.

Also Read
Mdahalo wa wagombea wenza wa Urais kuandaliwa Jumanne Juma lijalo

Waathiriwa wote 12 ni raia wa Kenya huku watano kati yao wakiwa wanaume na saba wakiwa wanawake. Mwathiriwa mchanga zaidi ana umri wa miaka 24, huku mkongwe zaidi akiwa na umri wa miaka 79.

Kaunti ya Nairobi ilinakili visa 10, huku kaunti ya kisumu na Tharaka nithi zikiandikisha kisa kimoja kila kaunti.

Also Read
Kenya yapokea dozi 200,000 za Sinopharm kutoka China

Wagonjwa 34 wamepona virusi hivyo, wote kutoka mpango wa kuwahudumia wagonjwa wakiwa nyumbani, na kufikisha idadi jumla ya waliopona Covid-19 hapa nchini kuwa 332,098

Kulingana na takwimu za wizara ya afya, idadi ya waliofariki kutokana ugonjwa huo hapa nchini ni 5,673. Kufikia sasa takriban chanjo milioni 20.9 zimetolewa nchini huku watu milioni 17.6 wakiwa wamechanjwa kikamilifu.

Also Read
Mzozo wa kinyumbani wasababisha mauti ya msichana wa miaka 8 Kilgoris

Takwimu za chuo kikuu cha John Hopkins zinaonyesha kuwa takriban visa milioni-589 vya mambukizi ugonjwa huo vimenakiliwa kote duniani huku watu milioni 6.4 wakifariki kutokana na makali ya ugonjwa huo.

  

Latest posts

Wetangula kuamua Alhamisi ni chama kipi kitashikilia wadhifa wa kiongozi wa wengi bungeni

Tom Mathinji

Gavana Orengo awatuma maafisa wakuu wa kaunti kwa likizo ya lazima

Tom Mathinji

Kipchoge na Kipruto warejea nyumbani kutoka London

Dismas Otuke

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi