Kenya yanakili visa 1,259 vipya vya Covid-19

Watu 1,259 zaidi wamethibitishwa kuambukizwa virusi vya Covid-19 baada ya kupimwa kwa sampuli 8,081 zilizochunguzwa katika muda wa saa 24 zilizopita.

Kiwango cha maambukizi ya virusi hivyo sasa ni cha asilimia 15.6. Idadi jumla ya virusi hivyo hapa nchini sasa ni 2,132,355

kati ya idadi hiyo mpya, watu 1,224 ni raia wa kenya na 35 ni raia wa kigeni huku watu 630 wakiwa wanawake na 629 wakiwa wanaume. Mwathiriwa mchanga zaidi ni mtoto wa umri wa miezi tano na mkongwe zaidi ana umri wa miaka 107.

wagonjwa watano zaidi wamefariki kutokana na virusi hivyo huku kifo kimoja kikitokea katika muda wa saa 24 zilizopita huku hivyo vingine vikiripotiwa kuchelewa baada ya ukaguzi wa rekodi za hospitali katika tarehe tofauti mwezi wa Julai mwaka 2021. Idadi jumla ya vifo kutokana na Covid-19 hapa nchini sasa ni 3,931.

Jumla ya wagonjwa 1,469 wamelazwa katika hospitali mbali mbali kote nchini hukuwengine 3,965 wakitunzwa nyumbani.

Wagonjwa 185 wamelazwa katika kitengo cha wagonjwa mahututi ICU, 43 kati yao wakitumia mitambo ya kuwasaidia kupumua na 86 wanapokea hewa ya ziada ya Oxygen. Wagonjwa 56 zaidi wanachunguzwa.

Hadi kufikia tarehe 30 nwezi Julai mwaka 2021, jumla ya watu 1,723,727 wamechanjwa dhidi ya Covid-19 ambapo watu 1,062,413 walichanjwa katika awamu ya kwanza na 661,314 walichanjwa katika awamu ya pili.

  

Latest posts

Idadi ndogo ya wakazi wa Nairobi wajitokeza kuchanjwa dhidi ya COVID-19

Tom Mathinji

Watumishi wa Umma wahimizwa kushirikisha taasisi mbali mbali kufanikisha majukumu yao

Tom Mathinji

Kenya yapokea dozi 200,000 za Sinopharm kutoka China

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi