Taifa hili limenakili visa 13 vipya vya Covid-19 baada ya kupimwa kwa sampuli 1,816 katika muda wa saa 24 zilizopita. Kiwango cha maambukizi ya Covid-19 hapa nchini sasa ni cha asilimia 0.7.
Idadi jumla ya visa vilivyothibitishwa hapa nchini kufika sasa ni 323,952 kutoka kwa Idadi jumla ya sampuli 3,625,373 zilizochunguzwa tangu mwezi Machi mwaka 2020.
Kati ya visa hivyo, waathiriwa tisa ni raia wa Kenya na wanne ni raia wa kigeni, huku watano wakiwa wa kike na wanane wakiume.
Mwathiriwa mchanga zaidi ni mtoto wa umri wa miaka tano na mkongwe zaidi ana umri wa miaka 60.
Wagonjwa sita wamepona virusi hivyo, wote kutoka mpango wa kuwatunza wagonjwa nyumbani. Hii inafikisha Idadi jumla ya waliopona Covid-19 hapa nchini kuwa 318,116.
Hakuna mgonjwa ameripotiwa kufakiri kutokana na Covid-19 hapa nchini, huku Idadi jumla ya vifo kutokana na virusi hivyo hapa nchini ikisalia kuwa 5,649.
Kulingana na waziri wa afya Mutahi Kagwe, jumla ya wagonjwa sita wamelazwa katika hospitali mbali mbali kote nchini, huku wengine 181 wakitunzwa nyumbani.
Hakuna mgonjwa ambaye amelazwa katika chumba cha wagonjwa mahututi ICU. Wagonjwa wawili wanapokea hewa ya ziada ya Oxygen wakiwa katika wodi za kawaida.