kenya yanakili visa 139 vipya vya Covid-19

Taifa hili limenakili visa 139 vipya vya Covid-19 baada ya kupimwa kwa sampuli 5,487 katika muda wa saa 24 zilizopita.

Idadi jumla ya visa vya Covid-19 hapa nchini sasa imefika 99,769 kutoka kutoka kwa idadi jumla ya sampuli 1,148,030 zilizopimwa tangu mwezi Machi mwaka jana.

Kati ya visa hivyo vipya vilivyonakiliwa Ijumaa, 119 ni vya wakenya huku 20 ni vya raia wa kigeni.  Waathiriwa 90 ni wa kiume na 49 ni wa kike

Also Read
Wizara ya Afya yaripoti vifo 11 kutokana na COVID-19 na maambukizi mapya 73

Mwathiriwa mchanga zaidi ana umri wa miaka miwili huku mkongwe zaidi akiwa na umri wa miaka 85.

Wakati huo huo wagonjwa 137 wamepona ugonjwa wa covid-19, 27 kutoka mpango wa kuwahudumia wagonjwa nyumbani huku 110 wakiruhusiwa kuondoka katika taasisi mbalimbali za afya  nchini.

Idadi jumla ya waliopona Covid-19 hapa nchini sasa ni 82,866.

Mgonjwa mmoja wa Covid-19 amefariki hapa nchini katika muda wa saa 24 zilizopita na kufikisha idadi jumla ya waliofariki nchini kutokana na makali ya Corona kuwa 1,740.

Also Read
Wakenya wajiunga na jamii ya Waislamu kuadhimisha Eid al-Adha

Kwa sasa wagongwa 577 wa corona wamelazwa katika hospitali mbali mbali nchini na wengine 1,553 wamewekwa katika mpango wa utunzi wa wagonjwa nyumbani.

Kwa mujibu wa waziri wa afya Mutahi Kagwe, wagonjwa 27 wamelazwa katika chumba cha wagonjwa mahututi ICU, 16 wanatumia vipumulio na 10 wanapokea hewa ya Oxygen ya ziada huku mgonjwa mmoja akiwa angali anachunguzwa.

Also Read
Kongamano kuhusu ugatuzi laahirishwa

Kaunti ya Nairobi iliendelea kuongoza katika maambukizi mapya huku ikinaliki visa 81, Mombasa ilifuata kwa visa 13, Turkana visa 11 huku kwale na Laikipia zinakili visa 3 kila moja.

Kaunti za Isiolo,Nakuru,Bomet,Trans Nzoia,Nyeri na Migori zilinakili visa viwili kila moja huku Taita Taveta,Busia,Embu,Kiambu,Kisumu,Kajiado,Kericho,Siaya,Kitui,Machakos,Kilifi na Pokot Magharibi zikiwa na kisa kimoja kila moja.

  

Latest posts

Mwanafunzi ateketeza bweni kukwepa kufanya mitihani Tharaka Nithi

Tom Mathinji

Mahakama yamzuia Mohammed Badi kuhudhuria mikutano ya Baraza la Mawaziri

Tom Mathinji

IEBC yalenga kuwasajili wapiga kura wapya milioni sita kabla Uchaguzi Mkuu ujao

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi