Kenya yanakili visa 244 vipya vya covid-19, watu wawili zaidi waaga dunia

Taifa hili limenakili visa vipya 244 vya Covid-19 na kufikisha idadi jumla ya visa hivyo humu nchini kuwa 38,115.

Visa hivyo vinatokana na sampuli 3,707 zilizopimwa kwa muda wa saa 24 zilizopita.

Kwa mujibu wa taarifa ya wizara ya afya, jumla ya watu ambao wamepimwa virusi hivyo humu nchini kufikia sasa ni 540,308.

Kati ya visa hivyo vipya, 228 ni Wakenya ilhali 16 ni raia wa kigeni. 157 ni wa kiume na 87 ni wa kike.

Also Read
WHO: Covid-19 hausambazwi kupitia kuwanyonyesha watoto

Aliye na umri wa chini zaidi ni mtoto wa miezi mitatu na aliye na umri wa juu zaidi ni mzee wa miaka 85.

Kaunti ya Nairobi inaongoza kwa visa 63 ikifuatiwa na Nakuru kwa visa 58, Kisii visa 23, Garissa visa 16, Kisumu visa 14 na Mombasa visa 13.

Also Read
Serikali yaongeza muda wa kuhudumu wa Baraza la Kidini

Kaunti ya Kiambu imenakili visa 10, Busia visa 9, Trans Nzoia visa 7, Turkana visa 6 na kaunti za Kajiado na Kericho visa 5 kila moja.

Kaunti za Uasin Gishu, Narok, Laikipia na Siaya ziko na visa 2 kila moja huku kaunti za Kakamega, Marsabit, Bungoma, Meru, Murang√°, Nyeri na Tharaka Nithi zikinakili kisa kimoja kila moja.

Also Read
Wanafunzi wa gredi ya nne na darasa la nane kufanya mitihani ya utathmini

Wagonjwa 40 wamepata nafuu, kumi kati yao wakiruhusiwa kuondoka kutoka hospitali mbalimbali ilhali 30 walikuwa wakihudumiwa nyumbani.

Jumla ya wagonjwa waliopona ugonjwa huo humu nchini ni 24,621.

Hata hivyo wagonjwa wawili zaidi waliaga dunia na kufikisha jumla ya watu waliofariki humu nchini kutokana na Covid-19 kuwa 691.

  

Latest posts

Nyongeza ya bei za mafuta yapingwa Mahakamani

Tom Mathinji

Kenya yanakili visa 113 vipya vya COVID-19

Tom Mathinji

Wazazi wasema watatetea mtaala mpya wa Elimu wa CBC

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi