Kenya yanakili visa 28 vipya vya Covid-19 aina ya India

Nchi hii imenakili visa vipya 28 vya maambukizi ya virusi vya Covid-19  vilivyogunduliwa nchini India.

Visa hivyo 28 ni miongoni mwa vingine 431 vilivyobainishwa kutoka kwa sampuli 5,864 zilizopimwa.

Idadi jumla ya visa vilivyothibitishwa hapa nchini sasa imeongezeka hadi 169,356 huku jumla ya sampuli 1,792,939 zikiwa zimepimwa.

Kiwango cha maambukizi hata hivyo kimepungua hadi asilimia 7.4.

Also Read
Visa 870 vipya vya Covid-19 vyathibitishwa humu nchini

Kati ya visa hivyo vipya,410 ni Wakenya, ilhali 21 ni wageni, huku mgonjwa wa umri mdogo akiwa mtoto wa miezi minne,na wa umri mkubwa akiwa na miaka 90.

Wagonjwa wengine 31 wamepona, 23 chini ya mpango wa uuguzi wa nyumbani, na wanane kutoka vituo mbali mbali vya afya.

Idadi jumla ya wagonjwa waliopona sasa ni 115,844. Hata hivyo wagonjwa wengine 10 wameaga dunia kutokana na ugonjwa huo na kuongeza idadi jumla ya vifo hadi 3,097.

Also Read
Visa vipya 148 vya Covid-19 vyanakiliwa humu nchini

Wagonjwa 1,103 wamelazwa katika vituo mbali mbali vya afya nchini ,huku wengine 4,713 wakiuguzwa nyumbani.

Wagonjwa 113 wamelazwa katika chumba cha wagonjwa mahututi ICU, ambapo  24 Kati yao wanatumia mitambo ya kuwasaidia kupumua, 65 wanapokea hewa ya ziada ya Oxygen na 24 wangali wanachunguzwa.

Also Read
Rais Kenyatta akutana na Waziri kutoka Japan katika Ikulu ya Nairobi

Kulingana na wizara ya afya, hadi kufikia sasa watu 960,379 wamechanjwa dhidi ya Covid-19 kote nchini.

Kati ya Idadi hiyo watu  291,259 Wana umri wa miaka 58 na zaidi, 164,588 ni wahudumu wa afya, 151,127 ni walimu,  81,158 ni maafisa wa usalama huku 272,247 wakitoka katika viwango vingine.

  

Latest posts

Nyongeza ya bei za mafuta yapingwa Mahakamani

Tom Mathinji

Kenya yanakili visa 113 vipya vya COVID-19

Tom Mathinji

Wazazi wasema watatetea mtaala mpya wa Elimu wa CBC

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi