Kenya yanakili visa 511 vipya vya COVID-19

Watu 511 wamethibitishwa kuwa na virusi vya COVID-19 hapa nchini kutokana na sampuli 6,434 zilizopimwa katika muda wa saa 24 zilizopita.Idadi hiyo ni sawia na kiwango cha maambukizi cha asilimia 7.9 .

Kati ya visa hivyo, 503 ni vya wakenya na visa  vinane ni vya raia wa kigeni. Waathiriwa 256 ni wa kiume na 255 ni wa kike. Wa umri mdogo zaidi ni mtoto wa miezi kumi huku wa umri mkongwe zaidi akiwa na miaka 96.

Also Read
Wagonjwa wawili zaidi wafariki kutokana na Covid-19 hapa nchini

Jumla ya visa vya maambukizi vilivyothibitishwa hapa nchini sasa ni 243,456. Kaunti ya Nairobi inaongoza kwa visa 93 na kufuatiwa na Kiambu kwa visa 56. Kaunti ya Nakuru imenakili visa 39 .

Watu 1,018 zaidi wamepona kutokana na ugonjwa huo hapa nchini ambapo 810 walikuwa wakihudumiwa nyumbani na 208 wameruhusiwa kuondoka katika vituo mbali mbali vya afya kote nchini.Jumla ya watu waliopona kufikia sasa ni 231,958.

Also Read
Kenya yanakili visa 1,286 vipya vya COVID 19

Hata hivyo wagonjwa sita zaidi  wamefariki kutokana na ugonjwa huo ambapo vifo hivyo vyote viliripotiwa baada ya kufanyia ukaguzi nakili za vituo hivyo vya afya mwezi uliopita na mwezi huu. Idadi hiyo imefikisha 4,902 jumla ya watu waliofariki kutokana na ugonjwa wa Covid 19 hapa nchini.

Also Read
Netanyahu akanusha mashtaka ya ufisadi dhidi yake

Jumla ya watu 1,617 kwa sasa wamelazwa katika vituo mbali mbali vya afya kote nchini huku 4,447 wakitunzwa nyumbani.

Kulingana na waziri  wa afya Mutahi Kagwe, wagonjwa 148 wamelazwa katika chumba cha wagonjwa mahututi ICU, 99 kati yao wanatumia mitambo ya kuwasaidia kupumua na 35 wanapokea hewa ya ziada ya Oxygen.

Hadi kufikia sasa watu 3,081,610 wamechanjwa dhidi ya COVID-19 hapa nchini.

  

Latest posts

Ronald Koeman atimuliwa Barcelona baada ya kushindwa na Vallecano

Dismas Otuke

Mutahi Kagwe: Wahudumu wa afya wafeli katika somo la Kingereza

Tom Mathinji

Prof Magoha: Awamu ya kwanza ya ujenzi wa madarasa ya CBC kukamilika mwezi Aprili mwakani

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi