Kenya yanakili visa 531 vipya vya Covid-19

Kiwango cha maambukizi ya virusi vya Covid-19 hapa nchini kimepungua baada ya watu 531 kupatikana kuwa na virusi hivyo baada ya kupimwa kwa sampuli 8,154 katika muda wa saa 24 zilizopita.

Kiwango cha maambukizi sasa ni asilimia 6.5 kutoka asilimia 8.1 kilichonakiliwa siku ya Ijumaa.

Hata hivyo watu 20 zaidi wamefariki kutokana na virusi hivyo na kufikisha idadi jumla ya waliofariki hapa nchini kutokana na Corona kuwa 3,671.

Kati ya visa hivyo vipya vilivyonakiliwa, 515 ni raia wa Kenya na 16 ni raia wa kigeni ambapo 274 ni wa kiume na 257 ni wa kike.

Also Read
Wasi wasi Laikipia kufuatia ongezeko la maambukizi ya COVID-19

Mwathiriwa mchanga zaidi ni mtoto wa umri wa mwaka mmoja huku mkongwe zaidi akiwa na umri wa miaka 93.

Idadi jumla ya visa vya Covid-19 vilivyothibitishwa hapa nchini sasa ni 185,591 huku idadi jumla ya sampuli zilizofanyiwa uchunguzi ikiwa 1,978,155.

Kaunti ya Nairobi iliongoza kwa kunakili visa 185, Uasin Gishu 43, Busia 38, Kiambu 30 nazo Siaya, Kilifi na Nakuru zikiandikisha visa 28 kila kaunti.

kaunti ya Kisumu ilinakili visa 24, Migori 20, Kakamega 14 huku Nyamira na Kericho zikiandikisha visa 12 kila kaunti.

Homa Bay ilinakili visa 9, Kajiado 6, Laikipia 5, Vihiga 5, Kisii 4, Kwale 4, Taita Taveta 4, Nyandarua 4, Murang’a 4, Baringo 3, Kitui 3, Machakos 3, Meru 3, Turkana 3, Bomet 2, Bungoma 2, huku Kirinyaga, Mombasa, Narok, Nyeri na Pokot Magharibi zikinakili kisa kimoja kila kaunti.

Also Read
Waathiriwa 300 wa mkasa wa moto Kangemi wapata msaada kutoka kwa Ananda Marga Mission

Waziri wa afya Mutahi Kagwe alitangaza kuwa watu 276 wamepona Covid-19 hapa nchini katika muda wa saa 24 zilizopita ambapo 151 walikuwa wakitibiwa nyumbani na 125 kutoka taasisi za afya kote nchini.

Idadi Jumla ya waliopona Covid-19 hapa nchini sasa ni 126,956. kati ya idadi hiyo 91,701 walitoka katika mpango wa kuwahudumia wagonjwa nyumbani na 35,255 walitoka katika hospitali mbali mbali kote nchini.

Also Read
Kaunti ya Nairobi yapata naibu mpya wa gavana

Jumla ya wagonjwa 1,144 wamelazwa katika hospitali mbali mbali nchini huku 5,785 wakitibiwa nyumbani.

Wagonjwa 124 wamelazwa katika chumba cha wagonjwa mahututi ICU, 39 kati yao wanatumia vipumulio na 51 wanapokea hewa ya ziada ya oxygen. Wagonjwa 34 wangali wanachunguzwa.

Hadi kufikia sasa watu 1,468,908 wamechanjwa dhidi ya covid-19 kote nchini.

Kati ya idadi hiyo chanjo 1,016,190 zilitolewa katika awamu ya kwanza huku watu 452,718 wakichanjwa katika awamu ya pili.

  

Latest posts

Visa 394 vipya vya COVID-19 vyanakiliwa hapa nchini

Tom Mathinji

Chris Obure ana kesi ya kujibu kuhusiana na sakata ya Anglo Leasing

Tom Mathinji

Rais Kenyatta atoa wito wa kuongezwa kwa uwekezaji wa Kilimo

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi