Kenya yanakili visa vilivyopungua zaidi vya Covid-19

Kiwango cha maambukizi ya virusi vya Covid-19 hapa nchini kimeshuka hadi asilimia 2.2 siku ya Jumatatu, baada ya watu 54 zaidi kuthibitishwa kuwa na virusi hivyo katika muda wa saa 24 zilizopita kutoka kwa sampuli 2,501 zilizopimwa.

Waliopatikana kuambukizwa virusi hivyo ni wakenya 52 na raia wawili wa kigeni ambapo 30 walikuwa wa kike na 24 wakiume huku mwathiriwa mchanga zaidi akiwa mtoto wa jumri wa miaka miwili na mkongwe zaidi akiwa na umri wa miaka 93. Idadi jumla ya visa vilivyothibitishwa hapa nchini ni 248,515 kutoka kwa sampuli 2,537,382 zilizofanyiwa uchunguzi tangu mwezi Machi mwaka 2020.

Also Read
Serikali ya kaunti ya Siaya kufadhili vyama vya ushirika ili kuimarisha uchumi

Idadi hiyo mpya ya maambukizi ilitangzwa na waziri wa afya Mutahi Kagwe akiwa katika kaunti ya Murang’a alipoweka jiwe la msingi kwa ujenzi wa kituo kipya katika hospitali ya kaunti ndogo ya Kigumo.

Kagwe alisema taifa hili linakaribia kufungua kikamilifu uchumi wake kufuatia kushuka kwa visa vya maambukizi kutokana na shughuli ya utoaji chanjo kwa umma inayolenga kuangamiza virusi hivyo.
Waziri huyo alisema wizara ya afya ililenga kuwachanja watu milioni 5.8 kabla ya tarehe 20 mwezi Oktoba mwaka 2021 kuwiana na siku kuu ya mashujaa.

Also Read
Kenya kupokea chanjo dhidi ya COVID-19 aina ya Johnson and Johnson Ijumaa

“Tarehe 20 mwezi Oktoba, tunaadhimisha siku kuu ya mashujaa na ni jambo la kutia moyo kuadhimisha siku kuu hii tukiwa tunakaribia kufungua kikamilifu uchumi wa taifa hili baada ya watu wengi kuchanjwa. Tunajizatiti kuhakikisha watu milioni 5.8 wanachanjwa tunapoadhimisha siku kuu ya mashujaa,” alisema waziri huyo.

Hadi kufikia sasa asilimia 3.3 ya wakenya wamechanjwa dhidi ya Covid-19 huku jumla ya watu 3,627,280 wakiwa wamechanjwa kote nchini.

Watu saba zaidi wamefariki kutokana na makali ya Covid-19 hapa nchini na kufikisha idadi jumla ya waliofariki kutokana na Covid-19 hapa nchini kuwa 5,109.

Also Read
Majasusi wanamsaka afisa wa polisi mwanamke kwa kuwaua watu wawili

Hata hivyo watu 437 wamepona virusi hivyo ambapo 314 walitoka katika mpango wa utunzi wa nyumbani na 123 waliruhusiwa kuondoka katika vituo mbali mbali vya afya kote nchini.

Jumla ya watu 1,126 wamelazwa katika hospitali mbali mbali kote nchini na wagonjwa wengine 2,586 wanatunzwa nyumbani. wagonjwa 73 wamelazwa katika chumba cha wagonjwa mahututi ICU, 49 kati yao wanatumia mitambo ya kuwasaidia kupumua na 24 wanapokea hewa ya ziada ya Oxygen.

  

Latest posts

Ronald Koeman atimuliwa Barcelona baada ya kushindwa na Vallecano

Dismas Otuke

Mutahi Kagwe: Wahudumu wa afya wafeli katika somo la Kingereza

Tom Mathinji

Prof Magoha: Awamu ya kwanza ya ujenzi wa madarasa ya CBC kukamilika mwezi Aprili mwakani

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi