Kenya yang’aa kwenye tuzo za filamu Zanzibar

Tuzo hizo za filamu ziliandaliwa mwisho wa tamasha la kimataifa la mwaka huu wa 2021 la filamu Zanzibar. Tamasha hilo liliandaliwa kisiwani humo kati ya tarehe 21 na 25 mwezi huu wa Julai.

Filamu ya Kenya kwa jina “Mission to Rescue”, ilishinda tuzo ya filamu bora ya matukio halisi yaani “Best Feature Film” katika eneo la Afrika Mashariki. Mwelekezi wa filamu hiyo Gilbert Lukalia alikuwa mwingi wa furaha akitangaza ushindi huo kupitia mitandao ya kijamii.

Also Read
Shindano la Ashanti na Keyshia Cole laahiriswa tena

Mission to Rescue ilishinda pia tuzo ya muigizaji bora ambaye ni Melvin Alusa. Alusa ndiye mhusika mkuu kwenye filamu hiyo ambayo inahusu wanajeshi wa Kenya na ambayo iliandaliwa katika eneo la mpaka kati ya Kenya na Somalia. Anaigiza kama Captain Barasa.

Also Read
Mr. Macaroni aachiliwa kwa dhamana

Kundi la kipekee la oparesheni linaloongozwa na Captain Barasa linajiandaa kwa kazi itakayofuata wakati linapokea habari kwamba Naibu Kamishna wa Kaunti ametekwa nyara na wapiganaji wa kundi la Alshabaab na kwamba wapiganaji hao wako karibu na eneo lao la mazoezi. Papo hapo, Captain Barasa anaanza mikakati ya kupanga jinsi ya kuokoa naibi kamishna kutoka kwa Alshabaab.

Also Read
Eric Omondi apanua wigo anapotafuta mke!

Wazo kuu la filamu hiyo ni kudhuhirisha madhara ya vijana kuingizwa kwenye makundi ya wapiganaji kwa nia ya kumaliza ugaidi.

Wanaoigiza kwenye Mission to Rescue ni Melvin Alusa, Warsame Abdi, Abdi Yusuf, Emmanuel Mugo, Andreo Kamau, Abubakar Mwenda, Sam Psenjen, Anthony Ndung’u, Bilal Mwaura, Justin Mirichi, Abajah Brian, Melissa Kiplagat, Brian Ogola na Mwamburi Maole.

  

Latest posts

Betty Bayo Afichua Sura ya Mpenzi Wake

Marion Bosire

Mr. Seed Asimulia Safari Yake ya Muziki

Marion Bosire

Rick Ross Azungumzia Uhusiano Wake na Hamisa Mobeto

Marion Bosire

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi