Kenya yapigwa kitutu na Argentina London Sevens

Kenya imecharazwa pointi 26 kwa nunge na Argentina katika mechi ya pili ya kundi B ,kwenye msururu wa nane wa mashinda ya IRB wa London Uingereza Jumamosi Alasiri.

Also Read
Mvua ya vuli inayotarajiwa na wakulima wajiandae

Shujaa ilikuwa chini alama 12 kwa bila kufikia mwishoni mwa kipindi cha kwanza ,kabla ya kumiminiwa alama nyingine 14 kunako kipindi cha pili.

Also Read
Mulee arejea Kuifunza Harambee Stars kwa miaka mitatu

Ulikuwa ushinde wa pili mtawalia kwa Kenya baada ya kupoteza alama 14-17 na Ireland katika mechi ya ufunguzi.

Shujaa chini ya ukufunzi wa Damian McGrath watashuka uwanjani Jumamosi saa kumi na mbili jioni kwa mechi ya mwisho ya kundi hilo huku ikiwa haina matumaini ya kufuzu kwa robo fainali ya kombe kuu.

  

Latest posts

Malkia Strikers wabanduliwa mashindano ya dunia baada ya kipigo cha seti 3-1 na Puerto Rico

Dismas Otuke

Boubacar Kamara kutocheza kwa muda kutokana na Jeraha

Tom Mathinji

Kenya kukabana koo na Puerto Rico mechi ya mwisho ya kundi A mashindano ya dunia

Dismas Otuke

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi