Kenya yapokea chanjo 180,000 za Astrazeneca kutoka Ugiriki

Huku serikali inapojitahidi kukabiliana na ongezeko la maambukizi ya Covid-19 kwa kuimarisha zoezi la kuwachanja watu, taifa hili limepokea msaada wa dozi 180,000 za chanjo ya Astrazeneca kutoka Ugiriki Ijumaa asubuhi.

Kuwasili kwa dozi hizo hapa nchini ni hatua kubwa kwa nchi hii katika kufanikisha vita dhidi ya virusi hivyo hatari.

Also Read
Uhaba wa ARV nchini walazimisha kaunti kusambaziana akiba zilizobaki

Kuwasili kwa chanjo hizo kutoka Ugiriki kunafikisha Idadi jumla ya chanjo zilizopokewa hapa nchini kuwa 2,323,100.

Akizungumza katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta JKIA kwa niaba ya serikali, Willis Akwale ambaye ni mwenyekiti wa jopo linalosimamia usambazaji wa chanjo, alisema serikali inapania kutoa chanjo kwa wakenya milioni 10 kufikia mwezi Disemba mwaka huu 2021.

Also Read
Watu sita zaidi wafariki kutokana na Covid-19 hapa nchini

Akwale ametoa wito kwa wakenya kujitokeza kwa wingi kupata chanjo hiyo ili kusaidia kukabiliana na janga la Covid 19. Kenya itapokea dozi nyingine za chanjo hiyo kutoka Latvia katika siku zijazo.

Hadi kufikia tarehe tano mwezi Agosti mwaka  2021, jumla ya watu 1,768,519 walikuwa wamechanjwa dhidi ya Covid-19 kote nchini.

Also Read
Waumini wa Kisii walalamikia ongezeko la visa vya makanisa kuteketezwa

Chanjo ya kwanza ilitolewa tarehe tano mwezi Machi mwaka 2021 huku serikali za kaunti zikianza kuwachanja watu tarehe 8 mwezi Machi mwaka 2021.

Waziri wa Afya Mutahi Kagwe amedokeza kuwa chanjo zaidi zinatarajiwa kuwasili humu nchini ili kupiga jeki zoezi linaloendelea la kuwachanja watu.

  

Latest posts

Wanjigi: Kenya haina uwezo kuwapa wasio na ajira shilingi 6,000 kila mwezi

Tom Mathinji

Mwanaume ajitia kitanzi baada ya kuteketeza nyumba yake eneo la Gichugu

Tom Mathinji

Viongozi wa kaunti ya Murang’a wampendekeza Peter Kenneth kwa wadhifa wa naibu rais

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi