Kenya yapokea zaidi ya dozi 400,000 za chanjo ya Astrazeneca kutoka Uingereza

Kenya imepokea msaada wa chanjo 410,000 ya Astrazeneca-Oxford kutoka kwa serikali ya Uingereza.
Chanjo hizo ambazo ziliwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta siku ya Jumamosi alasiri, zilitolewa na Uingereza kupitia mpango wa COVAX.

Maafisa wa serikali wakiongozwa na waziri mwandamizi katika wizara ya afya Dkt Mercy Mwangani, naibu balozi wa Uingereza hapa nchini Josephine Gauld, mkuu wa kitengo cha afya wa shirika la UNICEF Yaron Wolman, na mwakilishi wa shirika la Afya duniani hapa nchini Dkt Rudi Eggers walipokea chanjo hizo.

Also Read
Moto mkubwa wawaua watu 42 nchini Algeria

“Serikali ya Kenya inaishukuru serikali ya Uingereza kwa msaada huo ambao utasaidia pakubwa katika kuwachanja raia wa Kenya dhidi ya Covid-19,” alisema Mwangangi.

Kwa mujibu wa Mwangangi, msaada huo unajiri wakati ambapo taifa hili linaendelea kuwachanja wakenya katika awamu ya pili akiongeza kuwa chanjo hizo zitahakikisha wahudumu wa afya, walimu na wahudumu wengine wanalindwa dhidi ya kuambukizwa Covid-19.

Kwa pande wake, naibu balozi wa Uingereza hapa nchini Josephine Gauld alisema ushirikiano kati ya Kenya na Uingereza ni wa miaka 30 na unazidi kuwa dhabiti kila siku.

Also Read
Wataalam wanaochunguza chimbuko la Covid-19 nchini China wakamilisha muda wa kujitenga

“Tunafurahia kuisaidia kenya kutoa awamu ya pili ya dozi dhidi ya Covid-19 kwa kutoa msaada wa chanjo hizi ili kuokoa maisha ya wakenya,” alisema naibu huyo balozi wa Uingereza hapa nchini.

Utoaji wa chanjo dhidi ya Covid-19 unatekelezwa hapa nchini kwa ushirikiano kati ya wizara ya afya, Shirika la afya duniani, shirika la UNICEF, Gavi pamoja na washirika wengine.

Serikali ya kenya kwa sasa inawapa kipaumbele walimu, wahudumu wa afya na wahudumu wengine muhimu katika awamu ya pili ya utoaji wa chanjo dhidi ya Covid-19.

Also Read
Kenya yanakili kiwango cha 3.1 cha maambukizi ya korona

“Shirika la UNICEF linafurahia kuisaidia kenya katika kusafirisha na kusambaza chanjo hizi dhidi ya Covid-19,” alisema mkuu wa kitengo cha afya wa UNICEF Dkt. Yaron Wolman.

Shirika la Afya duniani WHO, lilitoa wito kwa wananchi kuzingatia masharti yaliyowekwa ya kuzuia kusambaa kwa Covid-19.

“Tunashukuru msaada huu kutoka Uingereza, wahudumu walio katika mstari wa mbele wangali kupata chanjo ya awamu ya pili ya dozi dhidi ya Covid-19,” alisema mwakilishi wa WHO humu nchini Dkt. Rudi Eggers.

  

Latest posts

Idadi ndogo ya wakazi wa Nairobi wajitokeza kuchanjwa dhidi ya COVID-19

Tom Mathinji

Watumishi wa Umma wahimizwa kushirikisha taasisi mbali mbali kufanikisha majukumu yao

Tom Mathinji

Kenya yapokea dozi 200,000 za Sinopharm kutoka China

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi