Kenya yaripoti maambukizi mapya 80 ya COVID-19

Wizara ya Afya humu nchini imeripoti visa vipya 80 vya maambukizi ya COVID-19 baada ya kupima sampuli 3,733 katika muda wa masaa 24 yaliyopita.

Hadi sasa, jumla ya visa vilivyoripotiwa imefikia 99,162 kutokana na upimaji wa jumla ya sampuli 1,125,679 tangu kisa cha kwanza kuripotiwa mnamo mwezi Machi mwaka wa 2020.

Kulingana na taarifa ya Wizara ya Afya, visa hivyo vipya ni pamoja na Wakenya 62 na raia 18 wa kigeni.

Also Read
Wenye mapato ya chini wasazwa huku hatua ya kuwapunguzia wakenya ushuru ikitamatika mwakani

48 kati yao ni wanaume, ilhali 32 ni wanawake, wa kati ya umri wa miaka 11 hadi 81.

Kaunti ya Nairobi imeendelea kuongoza kwa visa 62, ikifuatwa na Meru kwa visa 4, Busia 3, Kwale 3, Kiambu 2, huku Kaunti za Kericho, Kilifi, Makueni, Mombasa, Nyandarua na Uasin Gishu zikiripoti kisa kimoja kimoja.

Also Read
India yahimizwa kutoa chanjo ya Astrazeneca kwa mataifa ya kigeni

Kufikia sasa jumla ya wagonjwa 699 wanahudumiwa katika vituo mbali mbali humu nchini huku wengine 1,642 wakiwa kwenye mpango wa uuguzi wa nyumbani.

Kati ya walio hospitalini, 30 wako kwenye vyumba vya wagonjwa mahututi ambapo 14 wanatumia vifaa vya kusaidia kupumua na 13 wanapokea hewa ya ziada ya Oksijeni.

Also Read
Rais Kenyatta azindua hospitali ya kisasa yenye vitanda 100

Wakati uo huo, watu 26 waliokuwa wakiugua COVID-19 wamepona, 24 kati yao walikuwa wakitibiwa nyumbani na wawili hospitalini. Jumla ya waliopona sasa ni 83,350.

Hata hivyo, wagonjwa wengine watatu wamethibitishwa kuaga dunia kutokana na ugonjwa huo na kufikisha idadi ya waliofariki humu nchini hadi 1,731.

  

Latest posts

Visa 394 vipya vya COVID-19 vyanakiliwa hapa nchini

Tom Mathinji

Chris Obure ana kesi ya kujibu kuhusiana na sakata ya Anglo Leasing

Tom Mathinji

Rais Kenyatta atoa wito wa kuongezwa kwa uwekezaji wa Kilimo

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi