Kenya yatemwa nje na CAF kushiriki mechi za kufuzu kombe la AFCON mwaka ujao

Shirikisho la kandanda barani Afrika limeitupa Kenya nje ya mechi za kufuzu kwa fainali za kuwania kombe la AFCON mwaka ujao,mechi ambazo ziliratibiwa kuanza mapema mwezi ujao.

Kenya,ambayo inatumikia marufuku ya FIFA tamgu mwezi Februari mwaka ,ilikuwa imepangiwa kucheza mchuano wa kwanza wa kundi C, kufuzu kwa fainali za mwaka ujao za AFCON dhidi ya Cameroon tarehe 4 mjini Yaounde .

Also Read
Zinedine Zidane abwaga manyanga Real Madrid

Harambee Stars ilikuwa imejumuishwa pamoja na timu za Namibia na Burundi kando na Cameroon katika mechi hizo za kufuzu .

Also Read
Berlin Marathon:Kipchoge avunja rekodi ya dunia kwa sekunde 30

Kenya ilikuwa imepewa makataa ya wiki mbili na FIFA kurejesha hali ya kawaida, kabla ya mchuano wao dhidi ya Cameroon ,ili marufuku hiyo iondolewe.

Yamkini CAF wamechukua hatua hiyo kufutia uamuzi wa waziri wa michezo Dkt Amina Mohammed kuunda kamati ya mpito ya watu 11 kuendesha soka nchini wiki iliyopita ,akishikilia msimamo kuwa kamwe hatalegeza kamba hadi aondoe uchafu wote ulio kwenye soka ya Kenya.

  

Latest posts

Amos Kipruto ashinda London Marathon huku Jepkosgei akimaliza wa pili kwa vipusa

Dismas Otuke

Malkia Strikers wabanduliwa mashindano ya dunia baada ya kipigo cha seti 3-1 na Puerto Rico

Dismas Otuke

Boubacar Kamara kutocheza kwa muda kutokana na Jeraha

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi