Kenya yathibitisha visa vitatu vya Omicron

Waziri wa afya Mutahi Kagwe amesema watu kadhaa wanaoingia humu nchini kupitia viwanja vya ndege wamethibitishwa kuwa na virusi vya corona aina ya Omicron.

Hata hivyo Kagwe amesema Kenya haijathibitisha kisa chochote cha virusi hivyo vilivyosambazwa humu nchini.

Hata hivyo waziri ana imani kuwa nchi hii inaweza kuepusha ongezeko la visa vya maambukizi vya virusi hivyo.

Also Read
Obiri ahifadhi taji ya mbio za nyika za KDF huku Kandie akivuliwa ubingwa

Wakati huo huo Kagwe amewataka magavana kuweka vifaa vya kutosha katika vituo vya matibabu katika maeneo ya kaunti ili kupunguza gharama ya huduma za afya hapa nchini.

Kagwe ambaye alikuwa akiongea wakati wa mkutano wa mashauriano na magavana mjini Mombasa alitoa wito wa kubuniwa kwa sera za afya ambazo zitaboresha hazina ya bima ya kitaifa ya matibabu NHIF.

Also Read
Idadi ya madaktari wanaoaga dunia nchini kutokana na Covid-19 yaongezeka

Waziri alisema vituo vya afya vya umma vinaweza kutoa huduma bora za afya kama vituo vya afya vya kibinafsi.

Kagwe aliwaambia magavana kuwa mapato yanayokusanywa kutoka vituo vya afya katika maeneo ya kaunti yanafaa kutumika kuboresha huduma za afya kwa manufaa ya wananchi.

Alitaja ufisadi kuwa kizingiti katika juhudi za kuboresha huduma za afya katika maeneo ya kaunti.

Also Read
Waliopewa zabuni za kuunda madawati ya shule watakiwa kuharakisha kazi hiyo

Kagwe alisema sheria ya halmashauri ya usambazaji dawa hapa nchini KEMSA itarekebishwa ili kuwaruhusu wadau wengine pia kusambaza dawa badala ya kuachia jukumu hilo halmashauri ya KEMSA pekee.

Waziri alisema hatua hiyo itatatua tatizo la uhaba wa dawa katika maeneo ya kaunti.

  

Latest posts

Kenya yaadhimisha wiki ya kimataifa ya kuwanyonyesha watoto

Tom Mathinji

Kituo cha malipo cha barabara ya Expressway Mlolongo chafungwa

Tom Mathinji

Makundi ya wakiritimba yalaumiwa kwa kuficha Mahindi

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi