Kenya yatuzwa taifa bora barani Afrika kwa Utalii

Shirika la ndege la Kenya Airways limepokea tuzo la shirika bora zaidi la ndege barani Afrika katika kiwango cha kibiashara na kiuchumi na pia shirika lililojitangaza vyema zaidi barani Afrika kwenye tuzo za usafiri duniani mwaka huu.

Mpango huo wa kimataifa unanuiwa kutambua na kutuza utendakazi bora katika sekta za usafiri na utalii huku ukizindua washindi wa bara Afrika kuwiana na siku ya kwanza ya kutoa tuzo kwa washindi barani Afrika.

Also Read
Kenya Airways na Congo Airways yatia saini mkataba wa ushirikiano

Kenya ilipigiwa upato kuwa kituo kinachoongoza barani Afrika kutokana na mandhari yake bora, wanyama pori na fuo maridadi.

Jiji la Nairibi lilitajwa kuwa kituo kinachoongoza kwenye usafiri wa kibiashara barani Afrika na jumba la mikutano ya kimataifa la Kenyatta lilipokea tuzo ya kituo bora cha mikutano na makongamano.

Also Read
Kenya kutumia shilingi bilioni 1.37 kununua chanjo ya Oxford-AstraZeneca

Katika sekta ya utalii, hoteli ya Fairmont Mount Kenya Safari Club ilituzwa hoteli bora barani Afrika ilhali hoteli ya Aberdare Country Club, ilituzwa kuwa hoteli yenye mazingira maridadi zaidi barani Afrika.

Also Read
KFC Yatangaza Tarehe za Soko la Mwaka Huu la Filamu la Kalasha

Washindi walitangazwa kwenye hafla iliyohudhuriwa na watu mashuhuri huko Bahamas.

Sherehe za kutoa tuzo za World Travel Awards zinachukuliwa kuwa fursa bora ya kujitangaza katika sekta ya usafiri ambazo uhudhuriwa na viongozi wa serikali na sekta ya usafiri, watu mashuhuri na vyombo vya habari vya kimataifa.

  

Latest posts

Dereva na Makondakta wawili watiwa nguvuni kwa kukiuka sheria za trafiki

Tom Mathinji

Watu wanne zaidi wameambukizwa Covid-19 hapa nchini

Tom Mathinji

Matabibu wataka Uchunguzi wa mipakani kuimarishwa kuzuia kuenea kwa Ebola

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi