Kenya yazindua mashine ya kujipima mwenyewe virusi vya Ukimwi

Serikali imezindua mashine ya kujipima mwenyewe virusi vya Ukimwi katika juhudi za kupunguza maambukizi ya virusi hivyo.

Akiongea katika Kaunti ya Kajiado kwenye sherehe ya kuadhimisha Siku ya Kukabiliana na Ukimwi Duniani, Katibu Mwandamizi katika Wizara ya Afya Dkt. Mercy Mwangangi amesema serikali inategemea teknolojia katika juhudi mpya za kukabiliana na virusi hivyo.

Kulingana na Dkt. Mwangangi, nchi hii imepiga hatua kubwa kubwa kwenye vita dhiid ya ugonjwa huo, lakini hatua zaidi zinapasa kupigwa…

Also Read
Jumla ya visa vya COVID-19 humu nchini vyazidi 100,000 huku watu 69 zaidi wakiambukizwa

Mashine hiyo ambayo iko katika awamu ya kufanyiwa majaribio inaambatana na huduma za kutoa ushauri nasaha kwa njia ya mtandao kupitia kwa kituo cha kupiga simu kilicho na wataalam wenye ujuzi.

Mwangangi ametoa wito wa juhudi za pamoja kwenye vita dhidi ya virusi vya Ukimwi. Amesema hatua zilizochukuliwa zimesaidia kupunguza vifo vinavyotokana na Ukimwi kutoka elfu 166 mwaka wa 2007 hadi 20,997 mwaka uliopita

Also Read
IEBC yazindua rasmi zoezi la uthibitishaji saini za BBI

Kwenye maadhimisho hayo, Serikai ya Kaunti ya Kajiado imezindua mpango wa kumaliza maambukizi ya virusi vya Ukimwi kutoka kwa mama hadi kwa mtoto na maambukizi ya ugonjwa wa zinaa wa kaswende ifikapo mwaka 2024.

Kwenye ujumbe wake, Mama Taifa Margaret Kenyatta amewarai wadau kuongeza juhudi zao kwenye vita dhidi ya Ukimwi humu nchini kwa kuwekeza katika mipango ya kuwalinda Wakenya walio katika hatari ya kuambukizwa .

Also Read
Serikali kutumia shilingi bilioni 1.8 katika awamu ya kwanza ya kuwachanja wakenya

“Kuna uhitaji mkubwa wa kuongeza juhudi za uhamasishaji na rasilimali za kuzuia na kutibu Ukimwi hasa miongoni mwa mwa vijana, na kuwalinda watu wanaoishi na virusi hivyo kutokana na unyanyapaa na kutengwa,” amesema.

  

Latest posts

Wafungwa watoroka katika gereza la Nanyuki usiku wa manane

Tom Mathinji

Visa 323 vipya vya COVID-19 vyathibitishwa hapa nchini

Tom Mathinji

Ujenzi wa reli kati ya Mai Mahiu na Longonot wakamilika

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi