Kero la utekaji nyara lahofisha wanafunzi kurejea shuleni Nigeria

Watoto millioni moja nchini Nigeria huenda hawatarejea shuleni kwa kuhofia ghasia na msusuru wa visa vya utekaji nyara na mashambulizi yaliyolenga watoto mwaka huu wa 2021.

Kulingana na umoja wa mataifa, zaidi ya wanafunzi elfu moja wametekwa nyara na makundi ya wahalifu ili kuitisha ridhaa katika majimbo ya Kaskazini na kati kati mwa Nigeria tangu mwezi Disemba mwaka 2020, huku wengi wao wakiwa bado hawajaokolewa.

Also Read
Moto wazuka katika kanisa la TB Joshua

Shirika la watato la umoja wa mataifa UNICEF linasema kumekuwa na visa 20 vya mashambulizi mwaka huu dhidi ya shule nchini Nigeria, ambapo zaidi ya watoto 1,400 walitekwa nyara na 16 kati yao walifariki.

Also Read
Safari bado! Davido

Shirika hilo lilisema zaidi ya watoto million 37 nchini Nigeria wanatarajiwa kuanza mwaka mpya wa masomo mwezi Septemba, ambapo inakadriwa kwamba watoto million moja wanahofia kurudi shuleni.

Also Read
Boungei, Kibao kipya cha Emmy Kosgei

Karibu wanafunzi 70 waliotekwa nyara yapata wiki mbili zilizopita waliachiliwa wiki hii kwenye jimbo la Zamfara kaskazini magharibi mwa taifa hilo, ambako jeshi limeanzisha operesheni dhidi ya makundi ya utekaji nyara.

  

Latest posts

Rais Kenyatta amwomboleza Nancy Karoney, dadake waziri wa ardhi Farida Karoney

Tom Mathinji

Ronald Koeman atimuliwa Barcelona baada ya kushindwa na Vallecano

Dismas Otuke

Mutahi Kagwe: Wahudumu wa afya wafeli katika somo la Kingereza

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi