Kerrion Franklin Alaumu Mamake Akisema Anamdhulumu

Kerrion Franklin, ambaye ni kifungua mimba wa mwimbaji wa nyimbo za injili Kirk Franklin, amedai kwamba mamake huwa anamdhulumu, miezi kadhaa baada ya kutoa madai sawia dhidi ya babake.

Alitoa madai hayo Kupitia Instagram ambako alikuwa mubashara huku akionyesha mamake mzazi kwa jina Shawn Ewing na mwanamke mwingine wakiwa wamesimama mbali kidogo.

Also Read
Suzanna Owiyo anaomboleza

Kwenye video hiyo ambayo ilisambazwa mitandaoni, Kerrion wa umri wa miaka 33 anasikika akisema kwamba mamake anamdhulumu na kwamba aliamua kuja mubashara Instagram kutafuta usaidizi.

“Wanataka kunipeleka hospitali”, Franklin alisema na mamake akamjibu akisema ana mazoea ya kutafuta kuangaziwa mitandaoni.

Hapo ndipo alijitetea akisema anatafuta ulinzi Kwani mamake ambaye hana upendo kwake na Hana ukaribu naye anataka kumpeleka hospitali.

Also Read
Diamond Platnumz afanya ziara fupi nchini Kenya

Bi. Ewing anasikika akielezea kwamba aliitwa ili kusaidia kumpeleka mwanawe hospitali.

Mwezi Machi mwaka huu, Kerrion alitoa sauti iliyonakiliwa ya mvutano kati yake na babake Kirk Franklin ambayo ilizua minong’ono kote.

Kirk alisikika akimtupia mwanawe maneno ambayo wengi hawangetarajia kutoka kwa mwimbaji wa nyimbo za injili.

Also Read
Samidoh aomba msamaha

Baadaye Kirk Franklin alitoa video ambayo ilimwonyesha aliomba msamaha kwa kutumia maneno makali dhidi ya mwanawe na kuelezea safari ya malezi ya mtoto huyo wa kiume.

Kulingana naye Kerrion amekuwa na matatizo ya kiakili tangu alipokuwa mdogo na kama wazazi wamekuwa wakitumia pesa nyingi kwa matibabu yake.

  

Latest posts

Adasa Afichua Sababu ya Kimya Chake

Marion Bosire

Harmonize Matatani Tena

Marion Bosire

Pday Hurrikane Azungumzia Uhusiano Wake na Nyota Ndogo

Marion Bosire

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi