Kesi ya ufisadi dhidi ya Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu kurejelewa

Kesi ya ufisadi dhidi ya Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu imepangiwa kurejelewa, huku mahakama moja ya Jerusalem ikitarajiwa kupokea ushahidi kwa mara ya kwanza.

Netanyahu, mwenye umri wa miaka 71, anatuhumiwa kwa ulaji rushwaufisadi nkukiuka imani kuhusiana na kesi tatu tofauti.

Awali mwezi Februari, Netanyahu alikanusha mashtaka yote matatu dhidi yake.

Kesi yake imecheleweshwa mara kadhaa kwa ajili ya vikwazo vilivyohusishwa na janga la COVID-19 na pia uchaguzi mkuu wa mwezi uliopitaambapo iliangaziwa sana kwenye kampeini.

Kwa mara nyingine uchaguzi huo ulishindwa kutatua zogo lililodumu miaka miwili sasa nchini Israel, huku chama cha mrengo wa kulia chini ya uongozi wa Netanyahu na pia vyama vingine vya upinzani vikikosa kupata viti vinavyohitajika kuunda serikali.

Sasa Rais Reuven Rivlin wa nchi hiyo atashauriana na viongozi wa vyama wiki hiina baadaye kumteuwa yule ambaye anaamini ana fursa nzuri ya kuunda serikali mpya ya mseto.

  

Latest posts

Mzozo wa kidiplomasia kati ya Uchina na nchi za magharibi wasitishwa

Tom Mathinji

Watu saba wafariki katika mlipuko wa bomu nchini Somalia

Tom Mathinji

Shule nchini Uganda kufunguliwa Januari mwaka 2022

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi