Keter na Chepkirui washinda mita 1500 na kufuzu kwa mashindano ya dunia Kasarani

Vincent Keter na Purity Chepkirui ndio mabingwa wa kitaifa wa mbio za mita 1500 katika siku ya mwisho ya majaribio ya kitaifa kutea kikosi kwa mashindano ya dunia kwa chipukizi wasiozidi umri wa miaka 20 mapema Jumamosi uwanjani Kasarani.

Also Read
Rudisha atoa hamasa kwa vijana wa Kenya kujituma na kuhifadhi taji
Vincent Keter akiongoza mita 1500

Keter ambaye maajuzi amekosa tiketi ya kuelekea Olimpiki ametimka na kukata utepe kwa dakika 3 sekunde 38 nukta 85 naye Chepkurui akashinda zile za wanawake kwa dakika 4 sekunde 10 nukta 40.

Also Read
Brentford warejea EPL kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1947
Purity Chepkirui

Katika fainali ya mita 3000 Teresia Muthoni na Bernard Yegon wameibuka kidedea kwa wasichana na wavulana.

Chama cha riadha Kenya kinatarajiwa kutangaza kikosi cha Kenya ambacho kitaingia kambini baadae mwezi huu kujitayarisha kwa mashindano ya dunia baina ya Agosti 17 na 22 katika uwanja wa Kasarani ,Kenya ikitetea taji ya jumla waliyotwaa miaka mitatu iliyopita huko Tampere Finland kwa dhahabu 6 fedha 4 na shaba 1.

  

Latest posts

Wakenya Rotich na Tanui wavunja rekodi za Paris na Amsterderm Marathon

Dismas Otuke

Tusker waleweshwa nyumbani na Zamalek 1-0

Dismas Otuke

Tysa yasherekea miaka 20 ya kubadilisha vijana Kitale kupitia soka

Dismas Otuke

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi