Khloe Kardashian anaiga Beyonce?

Mwanamitindo wa Marekani Khloe Kardashian amebadili muonekano wake na ukimfananisha na Beyonce utaeleweka tu.

Nyota huyo wa kipindi cha familia yake almaarufu “Keeping Up With the Kardashians” ambaye ana umri wa miaka 36 amepata kazi ya kuwa sura ya mpango wa urembo kwa jina “Ipsy”.

Also Read
Blue Ivy ashinda tuzo la Grammy huku mamake akiandikisha rekodi mpya
Picha ya hivi punde ya Khloe kwenye Ipsy

Picha ambazo alipigwa kwa ajili ya kazi hiyo yake mpya ndizo zinazungumziwa kwani anaonekana tofauti kabisa na vile alikuwa akionekana awali.

Muonekano wake mpya ni kama wa Beyonce kwenye video ya wimbo “Bootylicious” wimbo ambao uliimbwa na kikundi ‘Destiny’s child’ na Beyonce alikuwa mmoja wao.

Also Read
"Uhalifu na Haki"
Muonekano wa Beyonce kwenye Video ya Wimbo “Bootylicious”

 

Khloe anaonekana mweusi kidogo kuliko kawaida na amevaa nguo za rangi ya “pink” ambayo huvutia macho kwa mbali.

Tofauti hiyo ya muonekano inaweza kuafikiwa kupitia kutumia bidhaa za urembo au kufanyiwa upasuaji wa urembo.

Also Read
Blue Ivy kuwania tuzo za Grammy

Haya yanawadia siku chache tu baada ya familia ya Kardashian kutangaza kwamba kipindi chao cha “Keeping Up with the Kardashians” kitafikia kikomo mwaka ujao.

  

Latest posts

Mwelekezi Sir Jacob Otieno Ameaga Dunia

Marion Bosire

Daddy Owen Azindua Albamu Mpya

Marion Bosire

Ogopa Wasanii, Kibao Kipya Cha Willy Paul

Marion Bosire

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi