Kibao Kipya cha Ringtone na Rose Muhando

Msanii wa nyimbo za injili Ringtone ametoa wimbo mpya ambao amemshirikisha Rose Muhando mwimbaji kutoka Tanzania. Wimbo huo unajulikana kama “Yesu Ang’are” na video yake ilitolewa kupitia You Tube tarehe 17 mwezi Septemba mwaka huu wa 2021.

Kwenye wimbo huo Ringtone anaimba akisema Yesu ang’are kwa sababu amemuinua baada ya kukatizwa tamaa na wengi kwamba hangefika mbali kama mwanamuziki. Muhando naye anaimba akisema Mungu ameaibisha wote waliokuwa kinyume nao na waliowanenea uwongo.

Also Read
Pigania Ndoa yako!

“Walinishusha umenipandisha, walinidharau Rose, ukaniinua, wengine walinibeza, ukaniheshimisha, ukaniketisha pamoja na wakuu”, ndiyo baadhi ya maneno anayoimba Rose Muhando kwenye kibao hicho.

Also Read
Andrea Martin Ameaga Dunia

Hii sio mara ya kwanza Ringtone anamshirikisha Rose Muhando kwenye muziki, mwezi Septemba mwaka 2019 wawili hao walitoa wimbo mwingine kwa jina “Walionisema”. Kufikia sasa video ya wimbo huo imetizamwa zaidi ya mara milioni 6 kwenye You Tube.

Also Read
S2kizzy kufanya kazi na Amber Rose mwakani

Ringtone ameshirikiana na wanamuziki wengine kutoka Tanzania pia kama Christina Shusho katika kibao kiitwacho “Tenda Wema” na kingine kinajulikana kama “Omba”.

Ameimba pia na Martha Mwaipaja wimbo unaojulikana kama “Backslide”.

  

Latest posts

Ogopa Wasanii, Kibao Kipya Cha Willy Paul

Marion Bosire

Kipindi Cha Wendy Williams Kuendelezwa na Watangazaji Tofauti

Marion Bosire

“Upendo” Kibao Kipya Kutoka Kwa Zuchu Na Spice Diana

Marion Bosire

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi