KICD yastawisha mtaala wa masomo kwa wanafunzi wa gredi ya 5 wenye mahitaji maalum

Taasisi ya Kitaifa ya kubuni mitaala ya masomo (KICD) kwa sasa inasimamia mchakato wa kubaini vitabu vya kiada kwa wanafunzi wa gredi ya tano wenye mahitaji maalum.

Hayo yanafwatia kustawishwa na kuidhinishwa kwa vifaa vinavyohitajika ambavyo vitatumika kuanzia mwezi Julai, na mtalaa wa umilisi kuanza kutumika kwa wanafunzi wa gredi ya tano.

Also Read
Taasisi ya Mitaala, KICD, yakamilisha uchapishaji vitabu vya Gredi ya 5

Wanafunzi watakaonufaika na vifaa hivyo vya mtaala ni pamoja na wenye matatizo ya kusikia, kuona na ulemavu wa mwilini.

Kwenye taarifa kwa vyombo vya habari, Afisa Mkuu wa KICD Profesa Charles Ongóndo alisema kuwa watoto wenye mahitaji maalum watashughulikiwa kama wengine, ikiwa rasilimali za kutosha zitatengwa kwa lengo hilo.

Also Read
TSC: Hatujafutilia mbali shughuli ya uajiri wa Walimu

Naibu Mkurugenzi wa mipango maalum kwenye taasisi hiyo Grace Ngugi Maina alisema watoto wenye mahitaji maalum wanastahili kushughulikiwa kama watoto wengine kwa kupewa elimu bora.

Also Read
Kaunti ndogo mpya yabuniwa Laikipia kukabiliana na utovu wa usalama

Aidha, aliwatia moyo wazazi wa watoto kama hao, akiwataka kuwapa elimu kwa kuwa wana uwezo wa kufanya vyema kama wenzao.

  

Latest posts

Mwanafunzi ateketeza bweni kukwepa kufanya mitihani Tharaka Nithi

Tom Mathinji

Mahakama yamzuia Mohammed Badi kuhudhuria mikutano ya Baraza la Mawaziri

Tom Mathinji

IEBC yalenga kuwasajili wapiga kura wapya milioni sita kabla Uchaguzi Mkuu ujao

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi