Kimanzi atawazwa kocha bora wa ligi kuu mwezi Januari

Kocha  Francis Kimanzi wa klabu ya Wazito Fc ameshinda tuzo ya kocha bora wa mwezi Januari kwenye ligi kuu ya Kenya .

Kimanzi aliiongoza  Wazito kushinda mechi tano na kumpiku Robert Matano wa Tusker Fc aliyeibuka wa pili.

Also Read
Coutinho kusalia mkekani kwa miezi mitatu

Kimanzi  alianza vyema mwezi Januari  akisajili ushindi  wa mabao 2-1 dhidi ya Nairobi City Stars ,kabla ya kuwazima Afc Leopards goli 1 kwa sifuri na kutoka nyuma bao moja na kulaza Bidco United 2-1  na kurudia matokeo hayo dhidi ya  Nzoia Sugar  na kufunga mwezi huo kwa ushindi wa bao 1 -0 dhidi ya Kakamega Homeboyz.

Also Read
David Alaba kugura Munich mwisho wa msimu huu
Also Read
AFCON U 20 kuingia semi fainali Jumatatu

Tuzo hiyo aliyopewa Kimanzi inaambatana na hundi ya shilingi elfu 50 na ndiye kocha wa pili kutuzwa msimu huu baada ya Zedekiah Zico Otieno wa KCB kutangazwa mshindi wa mwezi Disemba.

 

  

Latest posts

Sportpesa kurejesha ufadhili michezo nchini Kenya

Dismas Otuke

Vidosho wa Kenya wapigwa dafrao na Msumbiji mashindano ya kikapu Afrika

Dismas Otuke

FKF yakatiza mkataba wa shilingi milioni 127 na Odibets

Dismas Otuke

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi