Kimeli na Cheptai waibuka mabingwa wa mbio za kilomita 10 za Bengaluru

Wakenya Nicholas Kimeli na Irene Cheptai wametwaa ubingwa wa makala ya mwaka huu ya mbio za kilomita 10 za Bengaluru nchini India mapema Jumapili huku wakivunja rekodi .

Kimeli ameshinda mbio za wanaume akiweka rekodi mpya ya dakika 27 na sekunde 38 akifuatwa na Tadese Worku wa Ethiopia kwa dakika 27 na sekunde 43 huku mshindi wa mwaka jana Kibiwott Kandie akimaliza katika nafasi ya tatu lwa dakika 27na sekunde 57.

Also Read
Mabondia wa Kenya Cosby Ouma,Joshua Wasike na David Karanja watemwa nje ya mashindano ya dunia

Kimeli amevunja rekodi yake Geoffrey Kipsang kamworor ya dakika 27 na sekunde 34 ambayo imedumu tangu mwaka 2014.

Cheptai amewaongoza Wakenya kunyakua nafasi nne za mwanzo akikata utepe kwa dakika 30 na sekunde 35,akifuatwa na Hellen Obiri kwa dakika 30 an sekunde 44 huku Joyce Chepkemei akimaliza wa tatau kwa dakika 31 na sekunde 59 naye Joyce Cherono akaambulia nafasi ya nne.

Also Read
Kenya yanakili visa 1,504 zaidi vya COVID-19

Cheptai amevunja rekodi yake Agnes Jebet Tirop iliyoandikishwa mwaka 2018 ya dakika 31 na sekunde 19.

Matokea Rasmi

Wanaume

 1. Nicholas Kipkorir Kimeli (KEN) 27:38.
 2. Tadese Worku (ETH) 27:43.
 3. Kibiwott Kandie (KEN) 27:57.
 4. Telahun Bekele (ETH) 28:02.
 5. Yasin Haji (ETH) 28:03.
 6. Emmanuel Kiprop (KEN) 28:18.
 7. Muktar Edris (ETH) 28:31.
 8. Mathew Kimeli (KEN) 28:34.
 9. Reynold Kipkorir (KEN) 28:46.
 10. Abel Sikowo (UGA) 28:59.
Also Read
Nicholas Kimeli Mkenya pekee aliyeshinda Rome Diamond League

Wanawake

 1. Irene Chepet Cheptai (KEN) 30:35
 2. Hellen Onsando Obiri (KEN) 30:44
 3. Joyce Chepkemei Tele (KEN) 31:47
 4. Faith Cherono (KEN) 31:59
 5. Tariku Alemitu (ETH) 32:04
 6. Faith Chepkoech (KEN) 32:05
 7. Tesfaye Nigsti (ETH) 32:19
 8. Esther Borura (KEN) 32:29
 9. Pauline Esikon (KEN) 32:38
 10. Prisca Chesnag (UGA) 32:42
  

Latest posts

Shikanda ahifadhi uenyekiti wa AFC Leopards

Dismas Otuke

Kalle Rovanpera atwaa ubingwa wa raundi ya Kenya mashindano ya WRC

Tom Mathinji

Ajali ya kwanza yatokea katika barabara ya Expressway

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi