Kiongozi wa kundi la waasi la ADF akamatwa nchini DRC

 Jeshi la Uganda limesema kuwa kiongozi mkuu wa waasi amekamatwa mashariki mwa Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo.

Jeshi hilo limesema kiongozi huyo Benjamin Kisokeranio ni kamanda wa mrengo wa Allied Democratic Forces (ADF).

Also Read
Watu 15 wakamatwa Afrika kusini kwa madai ya ufisadi yanayohusiana na mazishi ya Mandela

Maafisa wa kijeshi wanasema kuwa Kisokeranio alikamatwa katika jimbo la kusini mwa Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo la Kivu alipokuwa akiingia nchini humo kutoka Burundi, sehemu ambapo Kikosi cha ADF kimekuwa kikitekeleza mashambulizi ya mara kwa mara.

Also Read
Jeshi la Uganda kusalia DRC hadi litakapotokomeza kundi la ADF

Mnamo mwezi Novemba mwaka 2020, serikali ya Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo(DRC), ilikubali kuruhusu jeshi la Uganda kuvuka mpaka ili kukabiliana na waasi hao wa ADF ambao wanadaiwa kuwa na uhusiano na kundi la Islamic State.

Also Read
Umoja wa Mataifa watoa dola milioni 40 kushughulikia hali ya dharura nchini Ethiopia

Maafisa wa utawala nchini Uganda wanalilaumu kundi hilo la ADF kwa kuhusika na mashambulizi kadhaa ya bomu katika mji mkuu wa Uganda Kampala.

  

Latest posts

ECOWAS kuiwekea Burkina Faso Vikwazo

Tom Mathinji

Rwanda kufungua mpaka baina yake na Uganda

Tom Mathinji

Wakazi wa Kaskazini mwa Ethiopia waghubikwa na baa la njaa

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi