Kiongozi wa waasi wa Liberia Alieu Kosiah kushtakiwa nchini Uswizi

Kesi ya uhalifu wa kivita dhidi ya aliyekuwa kiongozi wa waasi nchini Liberia, Alieu Kosiah, inatarajiwa kuanza leo nchini Uswizi.

Kosiah ni raia wa kwanza wa Liberia kukabiliwa na mashtaka ya uhalifu wa kivita wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini humo kati ya mwaka 1989 na 1996.

Also Read
Salva Kiir atoa wito wa kudumishwa kwa amani duniani

Kesi hiyo ilikuwa imeratibiwa kuanza mapema mwaka huu lakini ikaahirishwa kutokana na chamuko la maambukizi ya COVID-19.

Waathiriwa wa ukatili wa Kosiah hawatatoa ushahidi mahakamani kutokana na kanuni za kudhibiti msambao wa COVID-19 lakini watatoa ushahidi wao mwaka ujao.

Also Read
Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Jonson ajitenga kwa hofu ya maambukizi ya COVID-19

Kosiah anakabiliwa na tuhuma za dhuluma za kijinsia, mauaji, ulaji nyama ya binadamu, kusajili watoto jeshini na kulazimisha raia kufanya kazi katika mazingira magumu, madai ambayo Kosiah ameyakana.

Also Read
Wakili wa Kabuga ataka mteja wake ashtakiwe katika mahakama ya Hague badala ya Tanzania

Vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Liberia vilidumu hadi mwaka wa 2003 ambapo takriban watu elfu 25 waliuawa mikononi mwa wanajeshi vijana.

  

Latest posts

Mgomo wa wahudumu wa afya wasababisha maafa Guinea Bissau

Tom Mathinji

Aliyekuwa Rais wa Algeria Abdelaziz Bouteflika azikwa Jijini Algiers

Tom Mathinji

Aliyekuwa Rais wa Algeria Abdelaziz Bouteflika amefariki

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi