Kipindi cha Grapevine cha KBC chashinda kwenye tuzo za Sanaa

Grapevine ni kipindi ambacho huangazia matukio mbali mbali kwenye ulingo wa sanaa na hata tamaduni.

Mwaka huu wa 2020 kipindi hicho kimenyakua tuzo la kipindi bora cha sanaa na utamaduni kwenye runinga chini ya tuzo za Sanaa almaarufu “Sanaa Theatre Awards”.

Tuzo za sanaa ziliasisiwa na mwanahabari ambaye pia ni mwandishi wa tamthilia George Orido.

Kipindi hiki cha Grapevine huangazia matukio kama vile mashindano ya ulimbwende, tamasha za humu nchini na hata kimataifa, vyakula mbali mbali, tamasha za kitamaduni, filamu na matukio mengine ya burudani.

Also Read
Mchekeshaji Njoro arejea

Hafla ya kutuza washindi iliandaliwa jumapili tarehe 20 mwezi Disemba mwaka huu wa 2020 katika ukumbi wa Sanaa “kenya National Theatre”.

Mtayarishi wa kipindi cha Grapevine Wycliffe Gorry anasema kwamba wanashukuru sana kwa kutambuliwa kwa kazi nzuri ambayo huwa wanafanya.

Also Read
Filamu kupelekwa mashinani

Kulingana naye, hawakufahamu kwamba walikuwa wameteuliwa kuwania tuzo lakini walikwenda kuangazia halfa ya kutuza washindi kama ilivyo kawaida ya kazi yao wakashtukia wakiitwa wachukue tuzo.

Gorry anasema mwaka 2020 umekuwa mgumu kwani hakujakuwa na tamasha nyingi kutokana na kufutiliwa mbali kwa mikusanyiko kama njia moja ya kuzuia kusambaa kwa covid 19.

“Tulikuwa tunatumia picha za awali kujenga kipindi kwani ilikuwa vigumu kukutana na wasanii na walengwa wengine. Tulitumia pia teknolojia ambapo mahojiano yalitekelezwa kwa njia ya kimtandao” Alisimulia Gorry.

Also Read
Mwanamuziki mashuhuri wa Mugithi aaga dunia

Kipindi cha Grapevine kilianzishwa mwaka 2005 na tangu wakati huo kimebadili watayarishi na wasimulizi mara kadhaa.

Grapevine huwa kinapeperushwa kila siku ya Jumatatu saa nne usiku na marudio ni jumanne saa nane mchana.

  

Latest posts

Wasanii Wanaowakilisha Kenya AFRIMA

Marion Bosire

Akothee Apata Mgeni wa Heshima Kwenye Hafla Yake

Marion Bosire

KFCB Yazuia Usambazaji Wa Filamu

Marion Bosire

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi