Kithure Kindiki ajiondoa katika ulingo wa kisiasa

Siku moja baada ya muungano wa Kenya Kwanza kumtangaza Rigathi Gachagua kuwa mgombea mwenza wa William Ruto katika uchaguzi mkuu ujao, Seneta wa kaunti ya Tharaka Nithi Kithure Kindiki ametangaza kuwa atajiondoa katika siasa baada ya uchaguzi mkuu wa tarehe 9 mwezi agosti mwaka huu.

Akiongea na wanahabari katika hoteli moja JijiniĀ  Nairobi, Seneta huyo alibainisha kuwa hatatetea kiti hicho au kuwania wadhifa wowote wa kisiasa kwenye uchaguzi mkuu ujao, lakini ataendelea kumfanyia kampeni naibu wa rais William Ruto.

Also Read
Kenya kupokea dozi milioni 24 za chanjo ya covid-19

Uamuzi wa Seneta huyo wa Tharaka Nithi, unajiri baada ya kupoteza wadhifa wa mgombea mwenza kwa mbunge wa Mathira Rigathi Gachagua.

Kindiki alikuwa amepigiwa upato wa kuwa mgombea mwenza wa Dkt William Ruto, akitajwa kuwa msomi na mpangaji mikakati wa kupigiwa mfano.

Also Read
Wito watolewa wa ukaguzi wa pesa zilizofadhili mchakato wa BBI

Muungano ya Kenya Kwanza unaoogozwa na naibu Rais Dkt William Ruto na ule kwa Azimio la Umoja kinara wake akiwa Raila Odinga, imewachagua wagombea wenza kutoka eneo la kati mwa nchi kwa dhana ya kuwavutia wapiga kura kutoka maeneo hayo, ikizingatiwa kuwa eneo hilo kwa mara ya kwanza katika siasa za nchi hii, halina mgombea wadhifa wa urais katika uchaguzi mkuu ujao.

Also Read
Wakili Paul Gicheru kuachiliwa kwa muda na mahakama ya ICC

Kithure Kindiki alikuwa mmoja wa mawakili wa naibu Rais William Ruto katika mahakama ya kukabiliana na uhalifu wa jinai ICC jijini the Hague.

  

Latest posts

Ajali ya kwanza yatokea katika barabara ya Expressway

Tom Mathinji

Rais Kenyatta akamilisha kongamano la Jumuiya ya Madola Rwanda

Tom Mathinji

Waziri Matiang’i: Tutakabiliana vilivyo na makundi ya Majambazi

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi