Kituo cha Afya cha Wajir chakosa kutumika licha ya kukamilika miaka 11 iliyopita

Kituo cha Afya cha Sabuli katika eneo bunge la Wajir Kusini kilichojengwa kwa gharama ya shilingi milioni 47 hakijaanza kutumika kwa madai kwamba mkandarasi aliyekijenga hajalipwa.

Mkandarasi huyo, Aden Yusuf, alisema walipewa zabuni na wakakamilisha ujenzi wa kituo hicho mnamo mwaka 2010 lakini kufikia sasa wamelipwa asilimia 40 pekee ya gharama ya ujenzi.

Also Read
Mahakama Kuu yaharamisha utoaji kadi za huduma namba

Vyumba vingi katika kituo hicho cha afya viko katika hali duni kutokana na kwamba havijatumika tangu kukamilika, huku mazingira ya kituo hicho yakisalia kama mahame.

Yuusuf alidai juhudi za kuitaka Wizara ya Afya kutatua zogo hilo zimeambulia patupu.

Also Read
Chama cha Ekeza chawafidia wanachama wake pesa walizowekeza

“Tunahitaji pesa zetu kwa sababu ni haki yetu, na wakazi wanahitaji huduma kutoka kituo hiki. Ninamsihi Waziri wa Afya atusaidie kupata pesa zetu na afungue kituo hiki ili wakazi wahudumiwe hapa,” akasema Yusuf.

Also Read
Kenya yalenga kupanua shughuli za kitalii hadi mashambani

Wakazi walioongea na wanahabari walisema wanalazimika kusafiri mwendo wa kilomita 75 ili kupata huduma za matibabu katika eneo la Habaswein.

Waliitaka serikali kupitia kwa Waziri wa Afya Mutahi Kagwe kukifungua rasmi kituo hicho ili kuwaondolea dhiki hiyo.

  

Latest posts

Kliniki mpya ya ugonjwa wa saratani yafunguliwa katika kaunti ya Nandi

Tom Mathinji

Rashid Aman: Chanjo zinazotolewa hapa nchini ni salama

Tom Mathinji

Kampuni ya sukari ya Nzoia yalaumiwa kwa kutowalipa wakulima

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi