Kituo cha kujumlisha kura cha Narok kimehamishwa hadi ukumbi wa Bomas

Tume huru ya Uchaguzi na uratibu wa mipaka humu nchini (IEBC), imehamisha oparesheni za kituo chake cha kujumlisha kura kwenye kaunti ya Narok, hadi katika ukumbi wa Bomas of Kenya kufuatia ukosefu wa amani katika kituo hicho cha Narok.

Also Read
NCIC yahuburi uvumilivu kabla ya uchaguzi

Katika taarifa kwa wana-habari siku ya Jumapili, msimamizi wa Uchaguzi kwenye kaunti ya Narok Dkt. Sidney Namulungu,  alisema kumekuwa na ukosefu wa amani katika kituo cha kujumlisha kura cha kaunti hiyo, na kwamba haitawezekana kutangaza mshindi wa Ugavana katika mazingira yaliyokuwepo sasa.

Also Read
Wakenya waonywa dhidi ya kutoa jumbe za kupotosha

Hivyo basi, Namulungu alisema matokeo ya uchaguzi wa gavana yatatangazwa katika kituo cha kitaifa cha kujumlisha kura kilichoko ukumbi wa Bomas of Kenya.

Also Read
Mdahalo wa wagombea wenza wa Urais kuandaliwa Jumanne Juma lijalo

Kituo cha kujumlisha kura cha kaunti ya Narok kilikuwa kimefunguliwa kwenye chuo kikuu cha Maasai Mara.

  

Latest posts

Wetangula kuamua Alhamisi ni chama kipi kitashikilia wadhifa wa kiongozi wa wengi bungeni

Tom Mathinji

Gavana Orengo awatuma maafisa wakuu wa kaunti kwa likizo ya lazima

Tom Mathinji

Rais William Ruto ampokea Mpambe mpya

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi