Kituo cha kutibu magonjwa ya Figo chazinduliwa katika hospitali ya kitaifa ya Kenyatta

Ni afueni kwa wagonjwa wa fogo baada ya hospitali ya kitaifa ya Kenyatta kuzindua kituo kipya cha kushughulikia matatizo ya figo.

Hii ni hatua muhimu katika utekelezaji wa mpango wa afya kwa wote hasa kwa kutoa huduma za gharama nafuu za kushughulikia matatizo ya figo nchini.

Also Read
Ukusanyaji saini za BBI kuanza rasmi leo

Hatua hiyo ni afueni kwa watu wanaoathirika na maradhi ya figo nchini na katika kanda hii kwa jumla,  ambao wamekuwa wakilazimika kusafiri hadi katika mataifa kama India na Afrika kusini ili kutafuta matibabu.

Mkuu wa kitengo cha kushughulikia matatizo ya figo katika hospitali hiyo Dkt. Patrick Mbugua alisema kuzinduliwa kwa kituo hicho kipya kutasaidia kuboresha mafunzo na matibabu ya figo humu nchini na kuwasaidia wagonjwa kuepuka gharama kubwa za kutafuta matibabu nje ya nchi.

Also Read
Wanawake wanaougua Fistula kunufaika na Matibabu bila malipo katika hospitali ya Kenyatta

Akiongea wakati wa ziara hospitalini humo ya maafisa wa kitengo cha rais cha kufanikisha utekelezaji wa miradi muhimu, Dkt. Mbugua alisema kuwa kituo hicho kina uwezo wa kuwa na vitanda 16 huku kikitekeleza huduma mbalimbali zinazohusiana na upachikaji wa figo.

Also Read
Idadi ndogo ya wanafunzi wa kike yazua wasi wasi Nyanza na Magharibi

Dkt. Mbugua alisema kuwa wanapata matokeo kwa saa 24 katika kituo hicho kipya hali ambayo inafanya matibabu kuwa rahisi na ya gharama nafuu kwa wagonjwa.

  

Latest posts

Kamati ya Kusaidia Rais Mteule Kuchukua Hatamu za Uongozi Yaanza Kazi Rasmi

Marion Bosire

Didmus Barasa Ajisalimisha kwa Maafisa wa Polisi

Marion Bosire

Gavana Mandago Sasa ni Seneta

Marion Bosire

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi