Kiwango cha maambukizi ya Korona chafikia asilimia 5.9 humu nchini

Kiwango cha maambukizi ya ugonjwa wa COVID-19 hapa nchini kimeongezeka hadi asilimia 5.9 baada ya watu wengine 283 kupatikana na virusi hivyo kutokana na sampuli 4,822.

Wizara ya Afya pia imetangaza kwamba wagonjwa sita wamefariki katika muda was aa 24 zilizopita na kufikisha jumla ya maafa hadi 1,807.

Also Read
Shule ya Msingi ya Uhuru yafungwa baada ya wanafunzi kuambukizwa korona

Jumla ya maambukizi sasa imefikia 103,615, kutokana na upimaji wa jumla ya sampuli 1,254,018 tangu mwezi Machi mwaka jana.

Visa vilivyothibitishwa leo ni vya Wakenya 256 na raia 27 wa kigeni, wanaume 204 na wanawake 79.

Mgonjwa mwenye umri mchanga zaidi ni mtoto wa mwaka mmoja huku mkongwe zaidi akiwa na miaka 80.

Also Read
Evans Kidero aambukizwa Covid-19 wiki moja baada ya kuchanjwa dhidi ya virusi hivyo

Kaunti ya Nairobi imenakili visa 196, Busia 16, Kiambu 14, Mombasa 11, Nakuru 8, Uasin Gishu 6, Kajiado 5, Machakos 5, Kilifi 4, Kisumu 4, Kwale 3, Makueni 3, Homa bay 2, Taita Taveta 2, Murang’a 2, Siaya 1 na Migori 1.

Also Read
Janga la Covid-19 limezidisha visa vya ukataji miti kwa njia haramu nchini

Kulingana na wizara hiyo, wagonjwa 66 wamepona, 51 kutoka kwa uangalizi wa nyumbani na 15 kutoka hospitalini. Jumla ya waliopona sasa imefikia 85,457.

Kufikia sasa, wagonjwa 277 wanahudumiwa hospitalini na wengine 1,153 wanatunzwa nyumbani.

  

Latest posts

John Nkengasong: Omicron sio virusi vipya vya Covid-19

Tom Mathinji

Kenya yapokea dozi milioni 2 za chanjo aina ya AstraZeneca kutoka Ujerumani

Tom Mathinji

Watu 96 zaidi waambukizwa COVID-19 hapa nchini

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi