Kizz Daniel Akamatwa Nchini Tanzania

Oluwatobiloba Daniel Anidugbe maarufu kama Kizz Daniel ni mwanamuziki wa nchi ya Nigeria na taarifa za sasa zinaashiria kwamba amekamatwa na maafisa wa usalama nchini Tanzania. Kosa la mwimbaji huyo ni kukosa kutekeleza jukumu lake kulingana na mkataba kati yake na waandalizi wa tamasha.

Also Read
Vyombo vya Habari Tanzania Vyakatazwa Kucheza Wimbo wa Nay wa Mitego

Alikuwa amepangiwa kutumbuiza katika sehemu ya burudani iitwayo Warehouse jijini Dar es Salaam nchini Tanzania jana usiku lakini hakutokea. Waandalizi wa tamasha hilo wanasemekana kumripoti mwanamuziki huyo kwa maafisa wa polisi wakisema walipata hasara kubwa kutokana na mwanamuziki huyo kutofika tamasha I na tayari alikuwa amepokea malipo.

Also Read
Vipusa wa Pipeline,KCB na Prisons wafuzu kwa kwota fainali kombe la Afrika Voliboli

Video iliyochapishwa mitandaoni inaonyesha mwanamuziki huyo akishuka gari la polisi katika kituo cha polisi cha Oyster Bay jijini Dar nchini Tanzania. Mashabiki walikuwa wamenunua tiketi za tamasha hilo kwa bei ghali ambapo ya chini kabisa iligharimu elfu 80 pesa za Tanzania sawa na elfu nne za Kenya na ya juu ikigharimu laki moja unusu sawa na elfu saba na mia sita za Kenya.

Also Read
Rayvanny Achoma Nyumba Kisa Video ya Muziki!

Daniel kupitia Instagram alikuwa ametangaza tamasha hilo la Tanzania kupitia bango na mengine mawili nchini Rwanda na Malawi tarehe 13 na 27 mtawalia.

  

Latest posts

Watu wanne zaidi wameambukizwa Covid-19 hapa nchini

Tom Mathinji

Matabibu wataka Uchunguzi wa mipakani kuimarishwa kuzuia kuenea kwa Ebola

Tom Mathinji

Wabunge wa kaunti ya Kitui wataka baa la njaa kutangazwa janga la kitaifa

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi