Kocha na mchezaji wa zamani wa Shujaa Benjamin Ayimba afariki akiwa na umri wa miaka 44

Kocha wa zamani wa timu ya taifa ya raga kwa wachezaji 7 kila upande Benjamin Ayimba amefariki akiwa na umri wa miaka 44.

Kulingana na taarifa kutoka kwa msemaji wa familia Oscar Osir, Ayimba alifariki Ijumaa usiku katika hospitali kuu ya Kenyatta ambako amekuwa akipokea matibabu ya ugonjwa wa celebral malaria  kwa mwezi mmoja uliopita.

Also Read
Kenya Lionesses waendeleza mazoezi nchini Tunisia

Katika enzi zake marehemu alikuwa nahodha wa timu ya taifa ya raga kwa wachezaji 15 upande kabla ya kuingilia ukufunzi ambapo ameacha historia kuwa kocha aliyefanikiwa pakubwa akiwa na timu ya taifa ya raga kwa wachezaji 7 kila upande Shujaa  a,lipoiongoza kutwaa kombe kuu kwa ya kwanza na pekee mwaka 2016 kwenye msururu wa Singapore Sevens.

Also Read
Shujaa na Lionesses wabaini ratiba yao ya Madrid 7's

 

Ayimba aliteuliwa kuinoa Shujaa mwaka 2006 akiwa angali mchezaji wa timu ya taifa na awali alikuwa  ameshiriki kombe la dunia  kwa wachezaji 7 mwaka 2001 na 2005  na mwaka  2009 akaifuzisha Shujaa kwa fainali ya kwanza ya kombe  kuu mkondo wa Aadelaide na alipigwa kalamu mwaka 2011 kabla ya kurejeshwa  mwaka 2015  .

Also Read
Shujaa na Lionesses zamaliza nafasi za Pili Madrid 7's

Mola ailaze roho yake Benji mahala pema penye wema

  

Latest posts

Sportpesa kurejesha ufadhili michezo nchini Kenya

Dismas Otuke

Vidosho wa Kenya wapigwa dafrao na Msumbiji mashindano ya kikapu Afrika

Dismas Otuke

FKF yakatiza mkataba wa shilingi milioni 127 na Odibets

Dismas Otuke

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi