Kocha wa Gor Mahia Andreas Spier afunganya virago

Kocha wa klabu ya Gor Mahia Andreas Spier ameondoka Jumanne , baada ya kandarasi yake ya miezi sita na The Green Army kufutika .

Kocha huyo mwenye asili ya Ujerumani ni kocha wa tano kuinoa Kogalo ndani ya kipindi cha mwaka mmoja uliopita .

Also Read
Kombe la kifahari la dunia kuwasilishwa Nairobi Mei 26

Gor Mahia wamenolewa na makocha Carlos Manuel Vaz Pinto kutoka Ureno ,Sammy ‘Pamzo’ Omollo, Mwingereza Mark Harrison,Mganda Paul Nkata na hatimaye Spier tangu Januari mwaka huu na kufikisha jumla ya makocha 10 waliokuwa usukani tangu mwaka 2010.

Also Read
Martha Karua: Sitahudhuria mkutano wa UDA katika uwanja wa Kasarani
Also Read
Mdahalo wa wawaniaji Ugavana wa Nairobi kuandaliwa Jumatatu

Spier aliwaongoza Sirkal kumaliza katika nafasi ya tatu msimu uliopita kwa alama 54 ,pointi 9 nyuma ya mabingwa Tusker FC.

  

Latest posts

Msimu mpya wa ligi kuu ya FKF waahirishwa kutoka Oktoba Mosi

Dismas Otuke

Maendeleo ya Wanawake yampongeza Rais kwa kuwateuwa wanawake mawaziri

Dismas Otuke

KBC Channel One na Idhaa 13 kupeperusha mechi za kipute cha kombe la dunia

Dismas Otuke

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi