Kocha wa Gor Mahia Stephen Polack ang’atuka

Mabingwa wa ligi kuu nchini Gor Mahia wameanza sakasaka za mkufunzi mpya kufuatia kujiuzulu kwa Mwingereza Steven Polack.

Kwa mjibu wa barua iliyoandikwa na katibu wa kilabu Samuel Ochola,mabingwa hao mara 18 wa ligi kuu walikiri kupokea barua ya kujiuzu kutoka kwa Polack tarehe 8 mwezi huu huku wakielezea masikitiko yao na kumtakia kila la heri.

Also Read
Gor Mahia watemwa nje ya kombe la shirikisho baada ya kulazimishwa sare ya 1-1 na AS Otoho D Oyo

Polack aliye na umri wa miaka 58 alitarajiwa kurejea nchini Jumapili iliyopita baada ya likizo ya siku 10 ,tangu alipoondoka Septemba 12 ,lakini ameandika barua ya kujiuzulu kwa usimamizi wa Kogalo Ijumaa jioni.

Also Read
Shelly Ann Fraser Pryc aangazia mashindano ya dunia mjini Oregon baada ya kuweka muda wa kasi Kenya

Yamkini sawia na watungulizi wake wa kigeni huenda Polack aliamua kuibwaga manyanga ya Gor kwa kutolipwa kwa kipindi kirefuakiwa Kogalo ambapo aliwasaidia kunyakua taji ya ligi kuu msimu wa mwaka 2019/2020.

Polack alijiunga na Gor Agosti mwaka jana kutwaa nafasi ya Hasan oktay ambaye pia ling’atuka kwa njia ya kutatanisha baada ya kuwa likizoni barani ulaya.

Also Read
Mbappe asema angali na ndoto ya kucheza Real Madrid siku moja

Kogalo wataanza msimu mpya wa ligi pengine mwezi ujao bila kocha au wakiwa na kocha wa muda huku wakitafuta huduma za mkufunzi wa kigeni ilivyo desturi yao.

 

 

  

Latest posts

Takwimu za kipute cha 22 cha kombe la dunia nchini Qatar

Dismas Otuke

Sharon Chepchumba atua Ugiriki kupiga Voliboli ya kulipwa kwa miezi sita

Dismas Otuke

Boro wamtimua meneja Chris Wilder kwa matokeo duni

Dismas Otuke

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi