Kocha wa Shujaa Innocent Simiyu ana imani ya kupata maandalizi bora Kurume

Kocha wa timu ya taifa ya raga ya Kenya kwa wachezaji 7 kila upande, Innocent Simiyu ana imani timu hiyo itapata matayarisho bora mjini Kurume Japan inapojiandaa kwa michezo ya Olimpiki.

Timu hiyo iliripoti kambi ya mazoezi mapema wikii hii mjini Kurume.

‚ÄúNafikiria mazoezi yetu ya kwanza hayakuwa na msisimko kwa sababu wachezaji walikuwa wangali na maruerue kutokana na kusafiri na pia wangali hawajazoea hali ya anga,kuna mambo mengi ya kimsingi ambayo tutafanya nje ya uwanja ili kuimarisha mazoezi ya leo “akasema Simiyu.

Also Read
Malkia Strikers wajizatiti lakini waanguka seti 3-0 mikononi mwa wenyeji Japan

“Tuko na muda wa kutosha wa matayarisho na kile tutaangazia zaidi hapa ni mpangilio wetu wa mchezo”akaongeza Simiyu

Timu hiyo itakita kambi ya mazoezi mjini Kurume hadi tarehe 18,kabla kusafiri kwenda Tokyo Julai 19 .

Also Read
Mashemeji Ingwe na Kogalo kupimana nguvu fainali ya FKF CUP

Simiyu ana imani kuwa vijana wake watafanya vyema katika michezo ya Olimpiki licha ya kujumuishwa kundi gumu dhidi ya Ireland,USA na Afrika Kusini.

“Kundi letu ni gumu ,ukiangalia Ireland ni wazuri hata Japan wako poa baada ya kucheza hadi nusu fainali ya mwaka 2016,tutachukua kila mechi kwa wakati wakectukilenga kuonyesha umahiri wetu tukianzia na mchuano wa ufunguzi dhidi ya Afrika Kusini na Marekani ambayo itachezwa siku moja”

Also Read
Timu za raga kurejea kambini Kasarani wiki ijayo
Shujaa wakiwa mazoezini mjini Kurume

Shujaa watafungua kampeini ya Olimpiki Julai 26 dhidi ya Marekani na Afrika Kusini kabla ya kukamilisha mechi za makundi Julai 27 dhidi ya Ireland.

  

Latest posts

Sportpesa kurejesha ufadhili michezo nchini Kenya

Dismas Otuke

Vidosho wa Kenya wapigwa dafrao na Msumbiji mashindano ya kikapu Afrika

Dismas Otuke

FKF yakatiza mkataba wa shilingi milioni 127 na Odibets

Dismas Otuke

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi