Kongamano kuhusu ugatuzi laahirishwa

Kongamano la 7 kuhusu ugatuzi ambalo lilipangiwa kuanza Jumatatu juma lijalo limeahirishwa.

Uamuzi huo unafuatia hatua ya Rais Uhuru Kenyatta siku ya Jumatano, ya kutangaza masharti mapya ya kuzuia msambao wa ugonjwa wa Covid-19.

Rais Kenyatta aliagiza kusitishwa kwa mikusanyiko ya umma na pia mikutano yoyote baina ya watu kwa muda wa siku 60.

Also Read
Kenya yanakili visa 99 vipya vya Covid-19

Akiwahutubia wana-habari Alhamisi, mwenyekiti wa baraza la ma-gavana humu nchini Martin Wambora, alisema tarehe mpya za kongamano hilo la ugatuzi zitatangazwa baadaye.

Aidha, gavana huyo wa Embu alisema kongamano hilo ambalo lilikuwa limeratibiwa kufanywa kwenye shule ya upili ya wavulana ya Makueni kati ya tarehe 23 na 29 Augosti mwaka huu wa 2021 lingesababisha wanafunzi kuondoka mapema kwa likizo ya kati kati ya muhula.

Also Read
Zaidi ya maskwota 1,000 wafurushwa katika mpango wa makazi wa Chepchoina
Also Read
Uhuru Kenyatta: Afrika imepiga hatua kukabiliana na Malaria

Badala yake, wanafunzi hao sasa watapewa likizo yao kuanzia Jumatano tarehe 25 Augosti, na kurejea shuleni tarehe 3 Septemba.

Baraza hilo limewahimiza wakazi wa kaunti ya Makueni kuchukua fursa iliyopo ya kuchanjwa dhidi ya COVID-19 ili kulinda maisha yao.

  

Latest posts

Naibu Rais William Ruto akutana na Ujumbe wa waangalizi wa uchaguzi

Tom Mathinji

Kamati ya Kusaidia Rais Mteule Kuchukua Hatamu za Uongozi Yaanza Kazi Rasmi

Marion Bosire

Didmus Barasa Ajisalimisha kwa Maafisa wa Polisi

Marion Bosire

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi