Kongamano la Ma-jiji lafunguliwa rasmi Jijini Kisumu

Makala ya tisa ya kongamano la Ma-Jiji barani Afrika,  yalianza Jumanne asubuhi Jijini Kisumu.

Maudhui ya mwaka huu ni “Jukumu la Majiji ya kadri barani Afrika katika utekelezaji wa Ajenda ya maendeleo ya umoja wa mataifa kufikia mwaka 2030 na pia Ajenda ya maendeleo ya muungano wa Afrika kufikia mwaka 2063”.

Also Read
Kenya na Uingereza zaimarisha biashara baina yazo

Akifungua rasmi kongamano hilo Rais Uhuru Kenyatta alisema kwamba licha ya matatizo yaliyoletwa na janga la ugonjwa wa Covid-19, serikalki za kauntiz imetekeleza wajibu mkubwa katika kuzuia na pia kukabiliana na janga hilo.

Also Read
Rais Kenyatta kupokea mwili wa hayati Mwai Kibaki katika majengo ya bunge Jumatatu

Katika hotuba yake ya ufunguzi, Gavana wa Kisumu Profesa Anyang’ Nyong’o alisema kwamba majiji ya kadri kama vile Kisumu, yanatumika kama  mfano bora wa manufaaa ya ugatuzi. Alisema kongamano hilo limeandaliwa wakati ambapo maeneo ya miji yanashuhudia wimbi kubwa la wakaazi wa sehemu za mashambani kuhamia mijini.

Also Read
Rais Kenyatta awaalika hapa nchini wawekezaji kutoka Milki za Kiarabu

Hii ni mara ya kwanza ambapo Jiji la kiwango cha kadri limekuwa mwenyeji wa kongamano hilo.

Kenya imetunukiwa nafasi ya pili kuandaa kongamano hilo  baada ya kuandaa kongamano sawia mwaka 2006 jijini Nairobi. Kongamano hilo linahudhuriwa na wajumbe  4,500.

  

Latest posts

Kalle Rovanpera atwaa ubingwa wa raundi ya Kenya mashindano ya WRC

Tom Mathinji

Ajali ya kwanza yatokea katika barabara ya Expressway

Tom Mathinji

Cristiano Ronaldo kusalia Old Trafford

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi