Kora aelezea kilichomtoa “The Kansoul”

Mwanamuziki huyo ambaye awali alijiita Kid Kora ameamua kufunguka kuhusu sababu zake za kugura kundi la muziki la The Kansoul ambalo alisaidia kuanzisha.

Kupitia Insta Stories, mwanamuziki huyo ambaye ni kaka mdogo wa mwanamuziki Bamzigi alielezea kwamba alikuwa amechoka na maneno ambayo walikuwa wakitumia kwenye nyimbo zao kila mara ilhali walikuwa wamekuwa watu wazima na familia zao.

Also Read
Mejja amelishwa Kamote!

Anasema alisihi wenzake wawili ambao ni Madtraxx na Mejja wabadili mtindo wa kuimba lakini maneno yake yalipuuzwa. Kulingana naye, muda ulikuwa umewadia wa kuacha kuimba kuhusu ngono, kudhalilisha wanawake, pombe na shughuli kwenye sehemu za burudani.

Kid Kora aliachana na kundi hilo rasmi mwaka 2019 lakini hakuelezea sababu hadi sasa ambapo ameamua kufunguka akisema kuna pesa ambazo hakulipwa kwenye kundi hilo la The Kansoul.

Also Read
Tamasha la Jenga Jirani

Aliongeza kusema kwamba tangu aondoke kwenye kundi hilo, ameongeza uzani wa mwili na ngozi yake inang’aa na nywele zinamea ishara kwamba akiwa kwenye kundi hilo mambo hayakuwa sawa. Jambo lingine ambalo amezungumzia ni haja ya kulipwa hela zake kwani anasema amegundua kwamba alinyanyaswa upande wa hela.

Also Read
"Nitaendelea kusaidia mwanangu," asema Kirk Franklin

Isijulikane kama atachukua hatua za kisheria dhidi ya marafiki hao wake wa zamani au mambo yataishia tu kwenye mitandao ya kijamii.

Mwimbaji huyo alipachika pia picha yao watatu akisema yeye ndiye ana jina la kikora lakini wao ndio wakora kikweli.

  

Latest posts

Rihanna Sasa ni Billionaire!

Marion Bosire

Diamond amwombea mema Haji Manara

Marion Bosire

Bin Kalama kuzikwa Jumapili

Marion Bosire

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi