KRA: Miswada 23 iliyofutiliwa mbali na mahakama haitaathiri ukusanyaji ushuru

Mamlaka ya ukusanyaji ushuru nchini-KRA imetoa ufafanuzi kwamba  miswada iliofutiliwa mbali hivi majuzi haitaathiri shughuli ya ukusanyaji ushuru kwa kuwa ingali inatumika kwa mujibu wa mahakama.

Mahakama kuu ilibatilisha miswada 23 siku ya Alhamisi iliyokuwa imepitishwa na bunge la kitaifa bila kujumuisha bunge la Seneti.

Also Read
KRA yanasa shehena 43 zilizo na ngozi za thamani ya shilingi milioni 112

Hata hivyo mamlaka hiyo imesema kuwa hatua zilizochukuliwa za utekelezaji wake na mahakama ni halali.

Hii ni kwa sababu licha ya kubatilishwa,utekelezaji wa maagizo ya mahakama umesitishwa kwa muda wa miezi tisa  ili kumwezesha spika wa bunge la kitaifa na mwanasheria mkuu kuafikia kanuni za kifungu nambari 110 ibara ya 3 cha katiba na kuidhinisha utekelezaji wa sheria husika.

Also Read
Mahakama yazuia kuapishwa kwa Anne Kananu kuwa Kaimu Gavana wa Nairobi

Miswada  ya sheria iliyobatilishwa inayohusiana na usimamizi wa utozaji ushuru ni pamoja na  ile ya mwaka 2018 ibara ya 4,sheria ya mwaka 2018 ibara ya 9 kuhusu sheria ya utozaji ushuru,ile ya ibara ya 18  ya marekebisho ya sheria ya mwaka 2018 na  sheria kuhusu fedha ya mwaka 2018 ibara ya 10,miongoni mwa nyingine.

  

Latest posts

Mwanafunzi ateketeza bweni kukwepa kufanya mitihani Tharaka Nithi

Tom Mathinji

Mahakama yamzuia Mohammed Badi kuhudhuria mikutano ya Baraza la Mawaziri

Tom Mathinji

IEBC yalenga kuwasajili wapiga kura wapya milioni sita kabla Uchaguzi Mkuu ujao

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi