Kuahirisha chaguzi za Afrika kwafaa licha ya mizozo ya kikatiba asema Dkt Matsanga

Pendekezo la mahakama ya Afrika kushauri wanachama wa muungano wa Afrika AU, kuahirisha chaguzi zao kutokana na ugonjwa wa Covid 19 lazidi kuibua hisia mseto kutoka kwa wadau mbali mbali.

Mchanganuzi wa siasa za ukanda wa Afrika  Dkt david Matsanga anaunga mkondo pendekezo hilo ingawa anaona kuwa huenda likachangia mizozo ya kikatiba katika nchi nyingi.

Also Read
Shujaa kupambana na Ireland Jumatano kuwania nafasi ya 9 Olimpiki

Dkt Matsanga ana mtazamo kuwa huenda ikawa suluhu pekee kwani hali ya ugonjwa wa Covid 19 ilivyo kwa sasa inahofisha kutokana na mataifa mengi kushindwa kutoa chanjo ya virusi hivyo kwa  idadi kubwa ya wananchi wao ,mazingira  ambayo  hayataruhusu kampeini kufanyika kikamilifu ili kuruhusu  chaguzi za kidemokrasia.

Also Read
Kenya yaiparuza Niger seti 3-1 na kuweka miadi na Mali kuwania nafasi ya 9 mashindano ya Voliboli Afrika

Kenya inatarajiwa kuandaa uchaguzi wake mkuu mwezi Agosti mwaka ujao na kulingana na  Dkt Matsanga ni jambo la busara endapo uchaguzi ungeahirishwa ingawa itazua mzozo wa kikatiba.

Hapa nchini Kenya viongozi wengi wameteta wakisema kuwa hapana haja ya  kuahirisha uchaguzi mkuu wa mwaka ujao wakiwemo kiongozi wa Amani National Congress Musalia Mudavadi.

Also Read
IEBC yakanusha kuwa mifumo yake imedukuliwa

Ushauri huo  wa mahakama ya Afrika yenye makao yake jijini Daresalaam huenda ukayapata mataifa mengi katika njia panda ikizingatiwa kuwa zaidi ya  mataifa 58 yataandaa  chaguzi zao kuu mwaka ujao.

  

Latest posts

Nabulindo ashinda kesi ya kupinga kuchaguliwa kuwa mbunge wa Matungu

Dismas Otuke

Kenya yanakili visa vilivyopungua zaidi vya Covid-19

Tom Mathinji

Ibada ya wafu ya daktari Gakara na wanawe wawili yaandaliwa Nakuru

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi