Kundi la waasi lauteka mji wa Bangassou katika Jamhuri ya Afrika ya Kati huku mapigano yakiendelea

Kundi la waasi limeteka mji mmoja ulio Kusini Mashariki mwa Jamhuri ya Afrika ya Kati, kwa mujibu wa afisa wa ujumbe wa Umoja wa mataifa nchini humo.

Waasi hao walifanya shambulizi la alfajiri na kuuteka mji wa Bangassou, huku akisema mapigano yanaendelea katika badhi ya sehemu za nchi hiyo.

Also Read
Watu 10 wafariki katika shambulizi la bomu nchini Somalia

Muungano wa waasi nchini humo umekuwa ukishambulia miji kadhaa mnamo majuma ya hivi majuzi.

Waasi hao wanashtumu serikali kwa kufanya uchaguzi uliokumbwa na udanganyifu tarehe 27 mwezi Desemba, mwaka uliopita, madai ambayo serikali imeyakanusha.

Also Read
Guinea yaondolewa katika uanachama wa Muungano wa Afrika

Matokeo kamili ya uchaguzi huo wa urais na wabunge yanatarajiwa kutangazwa Jumatatu.

Serikali ya nchi hyo imemshtumu aliyekuwa rais wa nchi hiyo Francois Bosize, ambaye wanadai anasaidiwa na waasi kwa lengo la kufanya mapinduzi, lakini Bosize amekanusha madai hayo.

Also Read
Jamii ya kimataifa yaitaka Somalia kutatua zogo kuhusu uchaguzi mkuu

Siku ya Jumamosi, waasi hao walishambulia mji mwingine wa Damara, umbali wa kilomita 70 kutoka mji mkuu wa nchi hiyo Bangui.

  

Latest posts

Mgomo wa wahudumu wa afya wasababisha maafa Guinea Bissau

Tom Mathinji

Aliyekuwa Rais wa Algeria Abdelaziz Bouteflika azikwa Jijini Algiers

Tom Mathinji

Aliyekuwa Rais wa Algeria Abdelaziz Bouteflika amefariki

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi