KUPPET yapinga kozi za lazima za kutoa mafunzo kwa walimu

Maafisa wa tawi la Narok la chama cha taifa cha waalimu wa shule za sekondari na vyuo-KUPPET, wamepinga miito ya wizara ya elimu ya kuzindua kozi za lazima za mpango wa mafunzo wa kustawisha taaluma ya ualimu.

Also Read
Wito watolewa wa kubuniwa kwa afisi zaidi za usajili wa watu Garissa

Akiongea na wanahabari katibu wa tawi la Narok la chama cha KUPPET, Charles Ng’eno, alisema waalimu wataalam ambao hawataki mafunzo hayo hawajakosa tajriba kama anavyodai afisa mkuu wa tume ya kuwaajiri waalimu-TSC, Nancy Macharia.

Also Read
KUPPET :Walimu wapewe marupurupu ya kukabiliana wanafunzi watundu

Ng’eno alihoji kwanini tume ya TSC, imechagua vyuo vikuu vichache vya kibinafsi na kuviacha vile vya umma kutoa mafunzo hayo.

Also Read
Rais Kenyatta na Mama Taifa Margaret Kenyatta wachanjwa dhidi ya Covid-19

Mpango huo unawalenga waalimu elfu-340 kote nchini ambao watahitajika kuwasilisha upya vyeti vyao vya taaluma hiyo kila miaka mitano katika taasisi fulani.

  

Latest posts

Idara ya Mahakama yashutumiwa kwa kuhujumu shughuli muhimu za serikali

Tom Mathinji

Uhuru Kenyatta: Usalama wa taifa hili ni shwari

Tom Mathinji

Hospitali ya Kijeshi yazinduliwa katika kambi ya kijeshi ya Kahawa

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi