KUPPET :Walimu wapewe marupurupu ya kukabiliana wanafunzi watundu

Chama cha walimu wa shule za sekondari na vyuo nchini KUPPET kimeiomba serikali kuimarisha usalama wa Walimu wanaofunza katika maeneo yanayokabiliwa na utovu wa usalama nchini na pia kuanzisha marupurupu maalum kwa walimu wanaokabiliana na wanafunzi watundu maaru kama Rowdy Students allowance.

Also Read
Watahiniwa 287 hawatapokea matokeo ya mtihani wa KCSE

Akizungumza na KBC kwa mahojiano ya kipekee katibu wa KUPPET Akelo Misro amesema ni wakati mwafaka ambapo serikali inapaswa kutambua jukumu muhimu la walimu katika Jamii na kuboresha mazingira ya utendakazi wao ikiwemo kutoa ulinzi kwa wale wanaofunza katika maeneo yanayokabiliwa na vita mara kwa mara na pia kuanzisha marupurupu kwa walimu kwa minaajili ya kukabiliana na wanafunzi watundu.

Also Read
Chama cha walimu cha KNUT chalaumu kile cha KUPPET kwa kutotetea haki za walimu

Misori ameongeza kuwa likizo ndefu iliyotokana na janga la Covid 19 imesababisha wanafunzi kuingia na kujihusisha na makundi hatari na ndio chanzo cha visa vya hivi karibuni vya wanafunzi kuwaua au kuwajeruhi walimu.

Also Read
Kenya yanakili visa 664 vipya vya Covid-19

Chama cha KUPPET pia kimekamilisha maandalizi kwa uchaguzi wa kitaifa utakaondaliwa mapema mwezi April katika uwanja wa Kasarani baada ya uchaguzi wa mashinani kukamilika mwezi uliopita.

  

Latest posts

Rashid Aman: Chanjo zinazotolewa hapa nchini ni salama

Tom Mathinji

Kampuni ya sukari ya Nzoia yalaumiwa kwa kutowalipa wakulima

Tom Mathinji

China kupiga jeki uwezo wa kuzalisha chanjo hapa nchini

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi