KURA imepiga hatua kubwa kubadilisha taswira ya barabara za mijini asema Kinoti

Mkurugenzi mkuu wa mamlaka ya barabara za mijini KURA Silas Kinoti, ana imani kuwa wataafikia malengo ya kujenga ,kukarabati na kubadilisha mwonekano wa barabaraba zote za uma katika miji mikuu na manispaa kote nchini.

Kinoti akiwa usukani wa KURA tangu mwaka 2015 ,anajivunia ujenzi barabara mpya za kilomita 172 ,ukarabati wa nyingine kilomita 167.7 ,ujenzi wa madaraja 36 na ujenzi wa barabara unganishi pamoja na ujenzi wa barabara za wanaotembea kwa miguu umbali wa kilomita 288 nukta 8, na kilomita 9,797 zikiwekwa katika ukarabati wa mara kwa mara.

Also Read
Tatizo la mashamba lachelewesha mradi wa barabara Machakos

Ili kuafikia ajenda nne za serikali , barabara ni sekta muhimu kwa ukuaji wa uchumi kwa kuunganisha watu wa kutoka sehemu moja hadi nyingine na Kinoti anajivunia pia ongezeko la mali inayomilikiwa kupitia barabara kutoka shilingi bilioni 200 mwaka 2009 hadi shilingi Trilioni 1 kufikia leo.

“Mali inyomilikiwa kupitia barabara imeongezeka kila mwaka kutoka shilingi bilioni 200 mwaka 2009 na kufikia trilioni 1 hadi wa leo,ambayo imechangia kurahisisha usafirishaji wa watu na mizigo kuhakisha huduma za kijamii na mali ghafi imepatika ” amesema Kinoti Kura

Kulingana na mhandisi Kinoti kwa jumla KURA imetumia shilingi bilioni 69,195,742,095.91 kujenga kilomita 523 nukta 79 za barabara katika kaunti 27 ,kaunti ya Nairobi ikinufaika na kilomita 140 nukta 5 kwa gharama ya shilingi bilioni 48 nukta ikifuatwa na Kiambu iliyopata kiliomita 47 nukta 8 kwa zaidi ya shilingi bilioni 5 huku kaunti ya Meru ikipata kilomita 47 nukta3 za barabara .

Also Read
Unyakuzi wa ardhi watatiza ukarabati wa barabara ya Thika
Barabara ya Mandera iliyojengwa na KURA

Kura pia imeshirikiana pia na usimamizi wa kaunti ya Nairobi unaolenga kuboresha jiji kuu maarufu kama regeneration programme ambapo barabara za umbali wa kilomita 408 zitajengwa katika mitaa ya Dandora Utawala, Ruai, Mihang’o ikiwa umbali wa kimota 40, Dagoretti , Kangemi, Kawagware, Waithaka umbali wa kilomita 93 nukta 6, Kibra kilomita 22 nukta 8 ,Mathare kilomita 18 na kilomita 51 katika mitaa ya Royasambu , Zimmerman, Kahawa West na Gihurai miongoni mwa mitaa mingine jijini Nairobi .

Also Read
Nitatoka White House baadaye, Trump alegeza msimamo
Waziri James Macharia akiwa na  Mhandidi Kinoti wakikagua sehemu ya barabara ya Ngong  C

Ushirikiano wa kaunti ya Naiorbi na KURA utapunguza gharama ya ujenzi wa barabara kwani ujenzi huo hautakuwa ghali ikilinganishwa na ilivyo kuwa awali.

Kinoti ambaye alikuwa akihudumu kama kaimu mkurugenzi mkuu wa KURA tangu Septemba mwaka 2015 ,aliteuliwa kuwa mkurugenzi mkuu Juni 18 mwaka uliopita na waziri wa uchukuzi James Macharia.

  

Latest posts

Chissano atoa wito wa mazungumzo kati ya serikali na wapiganaji

Tom Mathinji

Vifo vya ndugu wawili vyazua taharuki Embu Kaskazini

Tom Mathinji

Gladys Erude ameaga dunia

Marion Bosire

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi